Chukua katika mali yake kwa wema, kiasi kinachokutosha wewe na wanao
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu kuhusu familia > Chukua katika mali yake kwa wema, kiasi kinachokutosha wewe na wanao
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Chukua katika mali yake kwa wema, kiasi kinachokutosha…
Maelezo ya hadith: Chukua katika mali yake kwa wema, kiasi kinachokutosha…
Alitaka kujua Hindu binti Utba radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mume wake Abuu Sufiani radhi za Allah ziwe juu yake, na kwamba yeye ni mwanaume bahili mwenye pupa sana na mali yake, hampi katika matumizi kiasi kinachomtosha yeye na wanaye, mpaka achukue katika mali yake kwa siri hali yakuwa hajui, je ana dhambi juu yake katika hilo?. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Chukua kwa ajili yako na watoto wako katika mali yake kiasi kinachojulikana katika mazingira ya kawaida na kwamba hicho ndicho kitakachomtosheleza hata asipojua.
Mafunzo: Chukua katika mali yake kwa wema, kiasi kinachokutosha…
- Uwajibu wa kutoa mahitaji kwa mke na watoto.
- Amesema bin Hajari: Na makusudio ya kauli yake: "Chukua katika mali yake kiasi kinachokutosha kwa wema", akamuelekeza katika wema kwa kiasi ambacho hakina kiwango katika sheria.
- Amesema bin Hajari: Hadithi hii imetumika kama ushahidi wa kuruhusu kumtaja mtu kwa yale asiyoyapenda ikiwa katika mfumo wa kuuliza na kulalamika na mfano wake, na hii ni moja kati ya sehemu ambazo hi halali ndani yake kusengenya.
- Amesema Qurtubi: Hindu hakukusudia kumsifia Abuu Sufiani kwa ubahili kwa hali zote, bali alieleza hali yake akiwa naye na kwamba yeye alikuwa akimtiadhiki yeye na wanaye, na hii haimaanishi ubahili wa moja kwa moja, kwani viongozi wengi hufanya hivyo kwa familia zao na huwaathiri sana upande wa kujenga mapenzi nao.
Makundi :
Fiq'hi- ufahamu- kuhusu familia.
· Matumizi.
· Fiq'hi na misingi yake.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
الله أكبر
Allah est le plus grand