Niacheni na vile nilivyo kuachieni, hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu kwa sababu ya …

Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Niacheni na vile nilivyo kuachieni, hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu kwa sababu ya …

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Niacheni na vile nilivyo kuachieni, hakika waliangamia…

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: «دَعُونِي مَا تَرَكْتُكُمْ، إِنَّمَا هَلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ بِسُؤَالِهِمْ وَاخْتِلَافِهِمْ عَلَى أَنْبِيَائِهِمْ، فَإِذَا نَهَيْتُكُمْ عَنْ شَيْءٍ فَاجْتَنِبُوهُ، وَإِذَا أَمَرْتُكُمْ بِأَمْرٍ فَأْتُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ».

Maelezo ya hadith: Niacheni na vile nilivyo kuachieni, hakika waliangamia…

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hukumu za kisheria zimegawanyika sehemu tatu: Zilizonyamaziwa, na makatazo, na maamrisho.

Ama ya kwanza: Nayo ni ile ambayo sheria imeinyamazia: Kiasi kwamba hakuna hukumu, nakuwa asili ya mambo huwasiyo wajibu kuyafanya; Ama katika zama zake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, ilikuwa ni lazima kujiepusha na kuuliza juu ya jambo ambalo halijatokea kwa kuhofia kuwekewa faradhi au katazo, kwani Mwenyezi Mungu aliliacha kwa ajili ya rehema kwa waja wake, na ama baada ya kufa kwake rehema na amani za Allah zimshukie, ikiwa swali liko katika mfumo wa fatwa au kujifunza kwa yale anayoyahitaji kuhusiana na mambo ya dini basi inajuzu bali imeamrishwa kufanya hivyo, na ikiwa ni katika namna ya jeuri na kuchimbua mambo, basi haya ndio maswali yanayokusudiwa kujiepusha nayo katika Hadithi hii. Na hii ni kwa sababu huenda ikapelekea katika yale yaliyowapata Wana wa Israeli, pale walipoamrishwa kuchinja ng'ombe yeyote lau wangelichinja ng'ombe yeyote basi wangelikuwa wametekeleza amri, lakini walitia mkazo, wakakaziwa pia.

Ya pili: Ni makatazo; nayo ni yale anayopata malipo mwenye kuyaacha, na anaadhibiwa mwenye kuyafanya, ni wajibu kuyaepeuka yote.

Ya tatu: Ni maamrisho; nayo ni yale anayopata malipo mwenye kuyafanya, na anaadhiwa mwenye kuyaacha, hivyo ni wajibu kuyafanya kwa kadiri ya uwezo.

Mafunzo: Niacheni na vile nilivyo kuachieni, hakika waliangamia…

Makundi : Msingi wa Fiq'hi. · Dalili za kimatamshi na namna ya kudadavua. · Akida- Itikadi- · Fiq'hi na misingi yake. · Kuamini mitume · Manabii na Mitume waliotangulia - juu yao amani.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله Gloire à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56