Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Nimepewa mambo matano ambavyo hakupewa mtu mwingine miongoni mwa Manabii kabla yangu
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu amempa mambo matano ambayo hakupewa yeyote katika Manabiii kabla yake:
La kwanza: Nimeepushwa na hofu, na hofu hiyo inatiwa katika nyoyo za maadui zangu hata kukiwa kati yangu na wao mwendo wa kutembea mwezi mzima.
La pili: Tumefanyiwa Ardhi kwetu kuwa Msikiti tuswali mahala popote tutakapokuwa, na udongo wake ni twahara (safi) pale tunaposhindwa kutumia maji.
La tatu: Tumehalalishiwa ngawira za vita, nazo ni zile wanazozichukua waislamu katika vita vyao na makafiri.
La nne: Nimepewa utetezi mkubwa katika kuwapumzisha watu na misukosuko ya kisimamo cha siku ya Kiyama.
La tano: Nimetumwa kuja kwa viumbe wote binadam wao na majini wao, kinyume na Manabii walikokuwa kabla yake, walikuwa wakitumwa kwa watu wao pekee.
Makundi : Akida- Itikadi- · Kuamini mitume · Mtume wetu Muhammad - Rehema na amani za Allah ziwe juu yake-