Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendezwa sana na kuanzia kulia, katika kuva…
Islam > Sw > Hadith > Historia ya mtume > Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendezwa sana na kuanzia kulia, katika kuva…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendezwa…
Maelezo ya hadith: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendezwa…
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akipenda na akipendelea kuanza na upande wa kulia katika mambo yake yanayostahiki heshima, na miongoni mwake ni: Kuanza na mguu wa kulia katika kuvaa viatu vyake, na kuanzia kulia katika kutana nywele za kichwa chake, kuziachanisha kwake na kuzipaka kwake mafuta, na katika kutawadha kwake, anatanguliza kulia kabla ya kushoto katika mikono na miguu.
Mafunzo: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendezwa…
- Amesema Imam Nawawi: Hii ni kanuni endelevu katika Sheria, kuwa kila jambo la heshima na utukufu kama vile kuvaa nguo, suruali, kandambili, kuingia msikitini, kupiga mswaki, kupaka wanja, kukata kucha, kupunguza masharubu, kuchana nywele, kung'oa nywele za kwapa, kunyoa kichwa, kutoa salam ya kumaliza swala, na kuosha viungo kwa ajili ya usafi, na kutoka nje ya choo, kula na kunywa, kupeana mikono, kugusa Jiwe Jeusi, na mambo mengine yenye kufanana na haya, basi ni sunna kuanza na upande wa kulia, na ama yale yaliyo kinyume chake, kama vile kuingia chooni, kutoka msikitini, kukidhi haja ndogo, kujisafisha, kuvua nguo, suruali, kandambili, na kadhalika, haya ni sunna kuanza na upande wa kushoto, na yote hayo ni kwa sababu ya heshima ya upande wa kulia na utukufu wake.
- "Anapendezwa na kuanzia kulia" Inajumuisha: Kuanza vitendo kwa mkono wa kulia, mguu wa kulia, upande wa kulia, na kushughulikia kitu kwa mkono wa kulia.
- Amesema Imam Nawawi: Tambueni kuwa miongoni mwa sehemu za udhu kuna ambazo hazipendezi kuanzia kulia; ambazo ni masikio, viganja, na mashavu, bali vitasafishwa vyote kwa wakati mmoja, ikiwa halitowezekana hilo kama ilivyo kwa mtu aliyekatwa sikio na mfano wake; basi atatanguliza upande wa kulia.
Makundi :
Historia ya Mtume.
· Mambo ya Mtume.
· Mavazi yake Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake:
· Muongozo wa Mtume.
· Historia na Taarekh.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
سبحان الله وبحمده
Gloire et louange à Allah