Wakati nikiwa natembea ghafla nilisikia sauti kutoka mbinguni, nikanyanyua macho yangu, gh…
Islam > Sw > Hadith > Historia ya mtume > Wakati nikiwa natembea ghafla nilisikia sauti kutoka mbinguni, nikanyanyua macho yangu, gh…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Wakati nikiwa natembea ghafla nilisikia sauti kutoka mb…
Maelezo ya hadith: Wakati nikiwa natembea ghafla nilisikia sauti kutoka mb…
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati akielezea kukatika kwa Wahyi na kuzuiwa kushuka kwake mwanzo wa kutumwa kwake: Wakati nikiwa natembea katika mitaa ya Makka ghafla nilisikia sauti kutoka mbinguni, nikanyanyua macho yangu, mara ghafla Malaika Jibril aliyenijia kule pango la Hiraa nikamuona amekaa juu ya kiti baina ya mbingu na Ardhi, nikapata hofu na fadhaa kwa sababu yake, nikarudi kwa familia yangu nikasema: Nifunikeni kwa nguo. Akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Ewe uliyejifunika nguo" uliyejigubika kwa nguo zako, "simama" kwa ajili ya kufikisha ujumbe "Uonye" na umtahadharishe asiyeamini utume wako. "na Mola wako Mlezi" Mungu wako muabudiwa "Umtukuze" na umhimidi na umtukuze. "Na nguo zako" na mavazi yako "yasafishe" yaondoshe najisi, "na machafu" kama kuabudu masanamu na mizimu "ihame" iache, Wahyi ukawa na nguvu baada ya hapo na ukakithiri.
Mafunzo: Wakati nikiwa natembea ghafla nilisikia sauti kutoka mb…
- Kukatika kwa Wahyi kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa muda kadhaa baada ya kuteremka kwa kauli yake Mtukufu: "Soma".
- Inafaa mtu kuzungumzia matukio yaliyomtokea baada kuisha kwake, kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu:
- Ya kwanza iliyoteremka ni kauli yake Mtukufu: "Ewe uliyejigubika" baada ya kuteremka: "Soma kwa jina la Mola Mlezi aliyeumba".
- Fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake kiasi kwamba alimmiminia wahyi wake pasina kukatika mpaka alipofariki.
- Uwajibu wa kusimamia kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuwaonya wapingaji na kuwapa habari njema watiifu.
- Uwajibu wa kusafisha nguo kwa ajili ya swala, na wametumia kama ushahidi kauli yake Mtukufu: "Na nguo zako zisafishe".
- Uwajibu wa kuamini Malaika na kwa yale aliyowawezesha Mwenyezi Mungu juu yake miongoni mwa matendo na mengineyo.
Makundi :
Historia ya Mtume.
· Prophet's Lineage
· Historia na Taarekh.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
اللهم صل على محمد
Ô Allah prie sur Muhammad