Alisema kuniambia mimi Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Soma
Islam > Sw > Hadith > Quran tukufu na elimu zake > Alisema kuniambia mimi Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Soma
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Alisema kuniambia mimi Mtume rehema na amani ziwe juu y…
Maelezo ya hadith: Alisema kuniambia mimi Mtume rehema na amani ziwe juu y…
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuomba Abdallah bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake amsomee chochote katika Qur'ani, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, vipi nikusomee na hali yakuwa Qur'ani iliteremshwa juu yako?! Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika mimi ninapenda kuisikia kutoka kwa mtu mwingine, akamsomea kutoka katika Suratun-Nisaai, alipofikia kauli yake Mtukufu: "Basi itakuwaje pindi tukiwaletea kutoka kila Umma shahidi, na tukakuleta wewe kuwa shahidi wa hawa". Yaani: Itakuwa vipi hali yako na hali ya Umma wako pindi tutakapokuleta kama shahidi juu ya Umma wako yakuwa wewe umewafikishia ujumbe wa Mola wako Mlezi, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Sasa, simama hapo katika kisomo chako, anasema bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake: Nikamgeukia ghafla nikaona macho yake yakibubujika machozi kwa hofu ya tukio hilo, na kwa kuuhurumia Umma wake.
Mafunzo: Alisema kuniambia mimi Mtume rehema na amani ziwe juu y…
- Amesema Nawawi: Sunna ya kusikiliza Qur'ani na kuitegea sikio na kulia wakati ikisomwa, na kuizingatia, na sunna ya kuomba kusomewa na mtu mwingine ili umsikilize, na hii ni njia bora zaidi ya kuielewa na kuizingatia kuliko mtu kusoma mwenyewe.
- Kuisikiliza Qur'ani kuna malipo sawa na kuisoma.
- Ubora wa Abdallah bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake, kiasi kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipenda kusikia kutoka katika kinywa chake, na hii inaonyesha pupa ya bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake juu ya kuitafuta Qur'ani na kuihifadhi na kuidhibiti vizuri.
- Fadhila ya kulia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu wakati wa kusikia aya zake, ikiwa ni pamoja na kuzingatia kunyamaza, na kimya kizuri, na kutopiga makelele.
Makundi :
Qur'an tukufu na Elimu zake
· Pekuzi za Qur'ani kiujumla.
· Adabu za Usomaji Qur'ani na Ubebaji wa Qur'ani.
بسم الله الرحمن الرحيم
mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
سبحان الله وبحمده
Gloire et louange à Allah