Mfano wa muumini mwenye kusoma Qur'ani ni kama mfano wa chenza harufu yake nzuri na ladha …

Islam > Sw > Hadith > Quran tukufu na elimu zake > Mfano wa muumini mwenye kusoma Qur'ani ni kama mfano wa chenza harufu yake nzuri na ladha …

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Mfano wa muumini mwenye kusoma Qur'ani ni kama mfano wa…

Maelezo ya hadith: Mfano wa muumini mwenye kusoma Qur'ani ni kama mfano wa…

Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake migawanyiko ya watu katika kuisoma Qur'ani na kunufaika nayo.

Sehemu ya kwanza: Ni muumini anayesoma Qur'ani na ananufaika nayo, yeye ni mfano wa chenza, lina ladha nzuri na harufu nzuri na rangi nzuri, na manufaa yake ni mengi, kwani yeye huyafanyia kazi anayoyasoma, na kuwanufaisha waja wa Mwenyezi Mungu.

Sehemu ya pili: Ni muumini asiyeisoma Qur'ani, yeye ni mfano wa tende, ladha yake tamu, lakini haina harufu, moyo wake umejawa na imani mfano wa tende ilivyojawa utamu katika ladha yake na juu yake, na kutosikika harufu yake ambayo watu huinusa; kwa kutosikika kisomo toka kwake ambacho watu watapata raha kwa kukisikiliza

Sehemu ya tatu: Mnafiki anayesoma Qur'ani, yeye ni mfano wa Ua Raihana, lina harufu nzuri na ladha yake chungu, kwakuwa hakuurekebisha moyo wake kwa imani, na hakuifanyia kazi Qur'ani, na anaonekana mbele za watu kuwa ni muumini, harufu yake nzuri inafanana na kisomo chake, na ladha ya chungu inafanana na ukafiri wake.

Sehemu ya nne: Mnafiki asiyeisoma Qur'ani, yeye ni mfano wa tango pori, kiasi kwamba halina harufu nzuri, na ladha yake ni chungu, kukosekana kwa harufu yake kumefanana na harufu yake; kwa kutoisoma, na uchungu wa ladha yake unafanana na uchungu wa ukafiri wake, ndani mwake kuko tupu hakuna imani, na nje yake hakuna manufaa, bali kuna madhara.

Mafunzo: Mfano wa muumini mwenye kusoma Qur'ani ni kama mfano wa…

Makundi : Qur'an tukufu na Elimu zake · Fadhila za Qur'an. · Ubora wa kuitilia umuhimu Qur'ani.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
اللهم صل على محمد Ô Allah prie sur Muhammad

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56