“Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika, hiyo ni sawa na theluthi m…
Islam > Sw > Hadith > Quran tukufu na elimu zake > “Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika, hiyo ni sawa na theluthi m…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: “Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake,…
Maelezo ya hadith: “Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake,…
Ameeleza Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake kwamba mtu mmoja alimsikia bwana mmoja akisoma suratu: "Qul-huwallaahu Ahad" akiikariri kila usiku na wala hazidishi sura nyingine, palivopambazuka alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamsimulia tukio hilo, ni kana kwamba muulizaji anaiona kuwa ndogo, akatoa kiapo rehema na amani ziwe juu yake kwa maana ya kuonyesha msisitizo, akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake hakika sura hiyo inalingana na theluthi ya Qur'ani.
Mafunzo: “Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake,…
- Fadhila za Suratul Ikhlaswi, na kuwa inalingana sawa na theluthi ya Qur'ani
- Inafaa kusoma katika kisimamo cha usiku walau kwa aya chache na kuzirudia rudia, na kutokuziona ndogo.
- Amesema Al-Maaziri: Inasemekana maana yake: Nikuwa Qur'ani iko katika sehemu tatu; visa na hukumu na sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na (Qul-huwallaahu Ahad) imejikita kwa ajili ya sifa za Mwenyezi Mungu, hivyo ni theluhti, na ni moja kati ya sehemu tatu, na imesemekana maana yake kuwa: Thawabu za kuisoma kwake hulipwa mara dufu kwa kiasi cha kusoma theluthi ya Qur'ani bila kuzidishwa.
Makundi :
Qur'an tukufu na Elimu zake
· Fadhila za Qur'an.
· Fadhila za Sura na Aya.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
أستغفر الله
Je demande pardon à Allah