Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa

Islam > Sw > Hadith > Quran tukufu na elimu zake > Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa

Maelezo ya hadith: Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa

Ameeleza Anas bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba alikuwa akitoa huduma ya vinywaji (pombe) kwa wale waliokuwa katika nyumba ya mume wa mama yake Abuu Twalha radhi za Allah za ziwe juu yake, na pombe yao wakati huo ilikuwa ni mchanganyiko, kati ya tende mbivu na tende mbichi, ghafla mnadiji wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akanadi: Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa, akasema: Anasema: Abuu Twalha akasema kuniambia, toka nenda kaimwage na uimimine, nikatoka nikaimwaga na nikaimimina, pombe ikatiririka katika mitaro ya Madina, wakasema baadhi ya watu: Wameuliwa baadhi ya Maswahaba na pombe ikiwa tumboni mwao ikiwa bado haijaharamishwa, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu:

"Hapana ubaya kwa wale walioamini na wakafanya matendo mema katika yale waliyokula". [Al-Maaida: 93] Mpaka mwisho wa aya. Yaani: Hawana dhambi wale walioamini katika vile walivyokula na kunywa katika pombe kabla ya kuharamishwa kwake.

Mafunzo: Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa

Makundi : Qur'an tukufu na Elimu zake · Vyakula na vinywaji. · Sababu za kuteremka aya · Vinywaji vilivyoharamishwa. · Fiq'hi na misingi yake. · Kuteremka Qur'ani na kukusanywa kwake.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
الحمد لله Louange à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56