Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu am…

Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu am…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila…

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إنَّ اللَّهَ طَيِّبٌ لَا يَقْبَلُ إلَّا طَيِّبًا، وَإِنَّ اللَّهَ أَمَرَ المُؤْمِنِينَ بِمَا أَمَرَ بِهِ المُرْسَلِينَ، فَقَالَ تَعَالَى: {يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنْ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا}، وَقَالَ تَعَالَى: {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ} ثُمَّ ذَكَرَ الرَّجُلَ، يُطِيلُ السَّفَرَ، أَشْعَثَ، أَغْبَرَ، يَمُدُّ يَدَيْهِ إلَى السَّمَاءِ: يَا رَبِّ! يَا رَبِّ! وَمَطْعَمُهُ حَرَامٌ، وَمَشْرَبُهُ حَرَامٌ، وَمَلْبَسُهُ حَرَامٌ، وَغُذِيَ بِالحَرَامِ، فَأَنَّى يُسْتَجَابُ لَذلك».

Maelezo ya hadith: Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila…

Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu ni mzuri na ni mtakasifu ametakasika na kila mapungufu na aibu na amesifika kwa yote yaliyokamilika, na wala hakubali katika matendo kauli na itikadi isipokuwa ile itakayokuwa nzuri, nayo ni ile iliyotakaswa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, yenye kwenda sambamba na muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na haitakiwi mtu ajikurubishe kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa hayo, na katika mambo yanayosababisha amali kuwa nzuri kwa muumini ni chakula chake kuwa kizuri, na kiwe kimetokana na halali, kwa hilo amali zake zinakuwa njema, na ndio maana Mwenyezi Mungu aliwaamrisha waumini kwa lile alilowaamrisha Mitume, ikiwemo kula halali na kutenda mema, akasema: "Enyi Mitume! Kuleni katika vilivyo vizuri na mtende mema, hakika mimi kwa yale mnayoyafanya ni Mjuzi" Na akasema: "Enyi mlioamini kuleni katika vizuri katika vile tulivyokuruzukuni".

Kisha akatahadharisha rehema na amani ziwe juu yake kula haramu,ambako kunaharibu matendo na kunazuia kukubalika kwake kwa sababu yoyote ile inayoonekana; ikiwemo:

Ya kwanza: Kuwa na safari ndefu iliyo katika misingi ya kumtii Mwenyezi Mungu kama Hija na Jihadi na kuunga udugu na mengineyo.

Ya pili: Nywele kukaa hovyo kwa kutotanwa, na kubadilika rangi ya ngozi na rangi ya nguo kwa sababu ya udongo, basi mtu huyu anakuwa kadharurika.

Ya tatu: Ananyanyua mikono yake juu mbinguni kwa dua.

Ya nne: Anamuomba Mwenyezi Mungu kupitia majina yake na anang'ang'ania katika hilo: Ewe Mola wangu Ewe Mola wangu!

Na pamoja na sababu hizi za kujibiwa dua hakusikilizwa; na hii ni kwa sababu chakula chake na kinywaji chake na mavazi yake ni vya haramu, na afya yake imetokana na haramu, ni mbali sana kwa mtu mwenye sifa kama hizi kujibiwa, na atajibiwa vipi?!

Mafunzo: Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila…

Makundi : Fiq'hi -Elimu- ya Dua na Dhikri mbali mbali. · Akida- Itikadi- · Sababu za Kujibiwa Dua. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima. · Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka · Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
اللهم صل على محمد Ô Allah prie sur Muhammad

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56