Alinifundisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake, namna ya tashahudi iletwayo ndani ya s…

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Alinifundisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake, namna ya tashahudi iletwayo ndani ya s…

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Alinifundisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake, nam…

عَنِ ابْنَ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: عَلَّمَنِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَكَفِّي بَيْنَ كَفَّيْهِ، التَّشَهُّدَ، كَمَا يُعَلِّمُنِي السُّورَةَ مِنَ القُرْآنِ: «التَّحِيَّاتُ لِلَّهِ، وَالصَّلَوَاتُ وَالطَّيِّبَاتُ، السَّلاَمُ عَلَيْكَ أَيُّهَا النَّبِيُّ وَرَحْمَةُ اللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ، السَّلاَمُ عَلَيْنَا وَعَلَى عِبَادِ اللَّهِ الصَّالِحِينَ، أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ».
وفي لفظ لهما: «إِنَّ اللهَ هُوَ السَّلَامُ، فَإِذَا قَعَدَ أَحَدُكُمْ فِي الصَّلَاةِ فَلْيَقُلْ: التَّحِيَّاتُ لِلَّهِ وَالصَّلَوَاتُ وَالطَّيِّبَاتُ السَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا النَّبِيُّ وَرَحْمَةُ اللهِ وَبَرَكَاتُهُ، السَّلَامُ عَلَيْنَا وَعَلَى عِبَادِ اللهِ الصَّالِحِينَ، فَإِذَا قَالَهَا أَصَابَتْ كُلَّ عَبْدٍ لِلَّهِ صَالِحٍ فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ، أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، ثُمَّ يَتَخَيَّرُ مِنَ الْمَسْأَلَةِ مَا شَاءَ».

Maelezo ya hadith: Alinifundisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake, nam…

Mtume Rehema na amani ziwe juu yake alimfundisha bin Masoud Radhi za Allah ziwe juu yake tashahudi inayosemwa ndani ya swala, akiwa kaweka mkono wake ndani ya mikono yake, ili asogeze karibu umakini wa bin Masoud. Na alifanya hivyo kama anavyomfundisha sura ndani ya Qur'ani jambo linaloonyesha kuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake aliitilia umuhimu tashahudi kwa matamshi na maana yake pia. Akasema: "Attahiyyaatu lillaah" (Maamkizi Mema ni ya Mwenyezi Mungu): Nayo ni kila kauli au kitendo kinachojulisha kutukuza, vyote hivyo vinastahiki kufanywa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Swala": Nazo ni swala zinazofahamika za Faradhi na za sunna zote hizo ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Mambo mazuri": Nayo ni maneno na matendo na sifa njema zinazojulisha ukamilifu, zote hizo zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Amani iwe kwako ewe Nabii na Rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake": Hii ni dua yake ya kuomba amani na uzima dhidi ya kila maafa na yenye kuchukiza, na kuomba ziada na wingi kutoka katika kila kheri. "Amani iwe juu yetu na kwa waja wema wa Mwenyezi Mungu": Hii ni dua ya kuomba uzima kwa kila mwenye kuswali na kwa kila mja mwema aliye mbinguni na ardhini. "Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu": Yaani ninakiri kukiri kwenye kuondoa shaka kabisa yakuwa hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu. "Na kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake": Ninakiri kwake kuwa ni mja na kapewa ujumbe wa mwisho.

Kisha akamhimiza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake mwenye kuswali achague katika dua aitakayo.

Mafunzo: Alinifundisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake, nam…

Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Sala. · Fiq'hi na misingi yake. · Sifa za Swala.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله وبحمده Gloire et louange à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56