Rudi kaswali, kwani wewe hujaswali

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Rudi kaswali, kwani wewe hujaswali

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Rudi kaswali, kwani wewe hujaswali

Maelezo ya hadith: Rudi kaswali, kwani wewe hujaswali

Aliingia Mtume rehema na amani ziwe juu yake msikitini, akaingia baada yake mtu mmoja akaswali rakaa mbili haraka haraka, na hakutulizana katika kisimamo chake na rukuu yake na sijida yake, na alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akimfuatilia katika swala yake, akaja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa kakaa pembezoni mwa msikiti, akamsalimia, akamjibu salamu, na akasema kumwabia: Nenda karudie swala; kwani wewe hujaswali. Akarudi na akaswali haraka kama alivyoswali mwanzo, kisha akaja akamsalimia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema kuwambia: Rudi kaswali; kwani wewe hujaswali, alifanya hivyo mara tatu. Yule bwana akasema: Namuapa yule aliyekutuma kwa haki, siwezi kufanya vizuri zaidi ya hivyo, basi nifundishe, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Utakaposimama katika swala basi toa takbira ya kuhirimia swala, kisha soma mama wa Qur'ani (Suratul-Faatiha) na kile atakachotaka Mwenyezi Mungu ukisome, kisha rukuu mpaka utulizane ukiwa umerukuu kwa kuweka viganja vyako juu ya magoti yako na unyooshe mgongo wako na umakinike katika rukuu yako, kisha nyanyuka na unyooshe mgongo wako mpaka mifupa irudi katika viungo vyake na ulingane sawa ukiwa wima, kisha sujudu mpaka utulizane ukiwa umesujudu kwa kuliweka sawa paji la uso na pua, na mikono miwili na magoti mawili na ncha za vidole vya miguu miwili juu ya ardhi, kisha nyanyuka mpaka utulizane ukiwa umekaa kati ya sijida mbili, kisha fanya hivyo katika kila rakaa ndani ya swala yako.

Mafunzo: Rudi kaswali, kwani wewe hujaswali

Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Sala. · Fiq'hi na misingi yake. · Sifa za Swala.

بسم الله الرحمن الرحيم mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
أحدب متناقص Gibbeuse Décroissante Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله Gloire à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56