Ewe Mwenyezi Mungu, usilifanye kaburi langu kuwa ni sanamu
Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Ewe Mwenyezi Mungu, usilifanye kaburi langu kuwa ni sanamu
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Ahmad
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Ewe Mwenyezi Mungu, usilifanye kaburi langu kuwa ni san…
عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم: «اللهُمَّ لَا تَجْعَلْ قَبْرِي وَثَنًا، لَعَنَ اللهُ قَوْمًا اتَّخَذُوا قُبُورَ أَنْبِيَائِهِمْ مَسَاجِدَ».
Maelezo ya hadith: Ewe Mwenyezi Mungu, usilifanye kaburi langu kuwa ni san…
Alimuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Mola wake asilifanye kaburi lake kuwa mithili ya sanamu lenye kuabudiwa na watu kwa kulitukuza, na kulielekea wakati wa kusujudu; kisha akaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi mungu yuko mbali na amemumfukuza na kumtowa kwenye rehema zake yeyote atakaye fanya makaburi ya manabii kuwa ni misikiti,kwani kulifanya kuwa msikiti ni njia ya kuelekea kuliabudu na kuliitakidi hivyo.
Mafunzo: Ewe Mwenyezi Mungu, usilifanye kaburi langu kuwa ni san…
- Kuvuka mpaka wa kisheria katika makaburi ya Manabii na watu wema hufanya yaabudiwe kinyume na Mwenyezi Mungu, ni lazima kuchukua tahadhari na njia zinazopelekea katika ushirikina.
- Haifai kwenda makaburini kwa lengo la kuyatukuza na kufanya ibada hapo, vyovyote vile utakavyokuwa ukaribu wa mwenye kaburi na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Uharamu wa kujenga misikiti juu ya makaburi.
- Uharamu wa kuswali makaburini hata kama hujajengwa msikiti hapo, isipokuwa swala ya jeneza ambalo halijaswaliwa (wanaweza kuswalia kwa dharura hiyo)
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Sala.
· Akida- Itikadi-
· Fiq'hi na misingi yake.
· Majina na Hukumu.
· Hukumu za Misikiti.
· Ushirikina.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
أستغفر الله
Je demande pardon à Allah