Swala ya mtu katika jamaa inazidi swala yake sokoni kwake na nyumbani kwake kwa daraja zai…

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Swala ya mtu katika jamaa inazidi swala yake sokoni kwake na nyumbani kwake kwa daraja zai…

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Swala ya mtu katika jamaa inazidi swala yake sokoni kwa…

Maelezo ya hadith: Swala ya mtu katika jamaa inazidi swala yake sokoni kwa…

Anaeleza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakaposwali muislamu katika jamaa, swala yake hiyo itakuwa bora kuliko swala yake nyumbani kwake au sokoni kwake kwa zaidi ya mara ishirini. Kisha akaeleza sababu ya hilo: Nayo nikuwa mtu atakapotawadha akatimiza vizuri udhu na ukaufanya vizuri, kisha akatoka kwenda Msikitini hakuna kinachomtoa ila kukusudia kusali, hatopiga hatua yoyote isipokuwa atanyanyuliwa kwa hatua hiyo daraja na nafasi ya juu, na hufutiwa kwake kwa hatua hiyo makosa, Atakapoingia Msikitini na akakaa akisubiri swala, basi atapata malipo ya swala na thawabu zake kwa muda wote atakaokaa akisubiri swala, na Malaika wakimuombea akiwa katika kikao chake aliposwalia, wakisema: "Ewe Mwenyezi Mungu msamehe, ewe Mwenyezi Mungu muhurumie, ewe Mwenyezi Mungu mfutie makosa" Huendelea kumuombea madam hajaharibu udhu wake, au akafanya yanayowakera watu au Malaika.

Mafunzo: Swala ya mtu katika jamaa inazidi swala yake sokoni kwa…

Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Sala. · Fiq'hi na misingi yake. · Ubora wa Swala ya Jamaa na Hukumu zake.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
حسبنا الله ونعم الوكيل Allah nous suffit, quel excellent protecteur

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56