Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mimi ndiye mtu niliyekaribu zaid…

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mimi ndiye mtu niliyekaribu zaid…

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, haki…

عن أَبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه: أنه كَانَ يُكَبِّرُ فِي كُلِّ صَلَاةٍ مِنَ الْمَكْتُوبَةِ وَغَيْرِهَا، فِي رَمَضَانَ وَغَيْرِهِ، فَيُكَبِّرُ حِينَ يَقُومُ، ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَرْكَعُ، ثُمَّ يَقُولُ: سَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَهُ، ثُمَّ يَقُولُ: رَبَّنَا وَلَكَ الْحَمْدُ، قَبْلَ أَنْ يَسْجُدَ، ثُمَّ يَقُولُ: اللهُ أَكْبَرُ حِينَ يَهْوِي سَاجِدًا، ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَرْفَعُ رَأْسَهُ مِنَ السُّجُودِ، ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَسْجُدُ، ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَرْفَعُ رَأْسَهُ مِنَ السُّجُودِ، ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَقُومُ مِنَ الْجُلُوسِ فِي الِاثْنَتَيْنِ، وَيَفْعَلُ ذَلِكَ فِي كُلِّ رَكْعَةٍ، حَتَّى يَفْرُغَ مِنَ الصَّلَاةِ، ثُمَّ يَقُولُ حِينَ يَنْصَرِفُ: وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، إِنِّي لَأَقْرَبُكُمْ شَبَهًا بِصَلَاةِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، إِنْ كَانَتْ هَذِهِ لَصَلَاتَهُ حَتَّى فَارَقَ الدُّنْيَا.

Maelezo ya hadith: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, haki…

Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- anapokea sehemu katika sifa ya swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na anaeleza kuwa alipokuwa akisimama katika sala anatoa takbira wakati ananyanyuka, nayo ni takbira ya kuhirimia swala, kisha anatoa takbira wakati anahama kwenda katika rukuu, na wakati anasujudu, na wakati anaponyanyua kichwa chake kutoka katika sijida, na wakati anasujudu sijida ya pili, na anaponyanyua kichwa chake kutoka katika sijida hiyo, na anaponyanyuka katika rakaa mbili za mwanzo baada ya kikao cha tashahudi ya kwanza katika swala yenye rakaa tatu au nne, kisha anafanya hivyo katika swala nzima mpaka anamaliza, na alikuwa akisema anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuu: Sami'allaahu liman hamidah, kisha anasema akiwa wima: Rabbanaa lakal hamdu.

Kisha anasema Abuu Huraira wakati anapomaliza swala: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mimi swala yangu iko karibu zaidi kufanana na swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- zaidi yenu, bali hii ndio ilikuwa sifa ya sala yake mpaka alipoondoka duniani.

Mafunzo: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, haki…

Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Sala. · Fiq'hi na misingi yake. · Sifa za Swala.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
الحمد لله Louange à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56