Fanyeni haraka kufanya matendo kuna fitina nzito kama kipande cha usiku wa giza,
Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Fanyeni haraka kufanya matendo kuna fitina nzito kama kipande cha usiku wa giza,
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Fanyeni haraka kufanya matendo kuna fitina nzito kama k…
Maelezo ya hadith: Fanyeni haraka kufanya matendo kuna fitina nzito kama k…
Mtume rehema na amani ziwe juu yake anamtaka Muumini kufanya hima na kufanya mambo mengi ya kheri kabla hayajashindikana, na akashughulishwa na kuja kwa fitna na mambo yenye kutatiza yanayoweza kuzuia kufanya matendo mema, na kuyaziba, na hali ni kwamba, ni giza kama kipande cha usiku ambao ndani yake haki imechanganyika na batili, na kukawawia vigumu watu kutofautisha baina yake, na kwa sababu ya ukali wake (Fitina hiyo), mtu huchanganyikiwa kiasi cha kuamka muumini, na kufika jioni ni kafiri, kushinda Muumini na kufika asubuhi kawa kafiri, anaiacha dini yake kwa starehe za muda mfupi za dunia.
Mafunzo: Fanyeni haraka kufanya matendo kuna fitina nzito kama k…
- Ni lazima kushikamana na dini, na kwenda mbio katika matendo mema kabla ya vikwazo kuzuia hilo.
- Hii ni ishara ya mfuatano wa majaribu yenye kupoteza katika zama za mwisho, na kwamba wakati wowote fitina moja inapotoweka, fitina ingine linafuata.
- Ikiwa dini ya mtu ni dhaifu na akaiacha kwa kubadilishana na mambo ya kidunia, kama vile pesa au vitu vingine, hii ni sababu ya kupotoka kwake, kuacha dini, na kuingia kwake kwenye vishawishi na fitina.
- Kuna ushahidi katika Hadithi kwamba matendo mema ni njia ya kuokoka na fitina.
- Kuna aina mbili za fitina: Fitina ya shubuha (Mambo yenye utata), na tiba yake ni elimu, na fitina ya matamanio, na tiba yake ni imani na subira.
- Hadithi inaashiria kuwa mwenye matendo kidogo, fitina kwake ni nyepesi zaidi, na mwenye matendo mengi anatakiwa asihadaike na alichonacho, bali aongeze zaidi.
Makundi :
Akida- Itikadi-
· Majina na Hukumu.
· Sehemu ya Imani.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
لا حول ولا قوة إلا بالله
Pas de force ni de puissance sauf en Allah