Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na haya zaidi kuliko hata bikira ndani ya chum…
Islam > Sw > Hadith > Historia ya mtume > Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na haya zaidi kuliko hata bikira ndani ya chum…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na haya zai…
Maelezo ya hadith: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na haya zai…
Anasimulia Abuu Said Al-Khudri Mwenyezi Mungu amuwie radhi, kuwa alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na haya zaidi kuliko msichana bikira ambaye hajaolewa na kuishi na wanaume aliyefichwa nyumbani kwake, na kwa sababu ya ukubwa wa aibu yake anapokichukia kitu uso wake unabadilika na wala hazungumzi, bali masahaba wake wanalibaini hilo katika uso wake.
Mafunzo: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na haya zai…
- Kumebainishwa miongoni mwa sifa alizokuwa nazo Mtume rehema na amani zimshukie kama haya, ambayo ni tabia tukufu.
- Haya ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, maadamu hayajatendeka makatazo ya Mwenyezi Mungu, yakitendeka basi rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akikasirika na kuwaamrisha maswahaba zake na kuwakataza.
- Himizo la kujipamba na sifa ya haya; kwa sababu huisukuma nafsi kufanya mazuri na kuacha machafu.
Makundi :
Historia ya Mtume.
· Mambo ya Mtume.
· Sifa za kitabia.
· Haya za Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake:
· Historia na Taarekh.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
سبحان الله وبحمده
Gloire et louange à Allah