Amesema Allah Aliyetakasika na kutukuka: Nimewaandalia waja wangu wema, vitu ambavyo jicho…
Islam > Sw > Hadith > Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha > Amesema Allah Aliyetakasika na kutukuka: Nimewaandalia waja wangu wema, vitu ambavyo jicho…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Amesema Allah Aliyetakasika na kutukuka: Nimewaandalia…
Maelezo ya hadith: Amesema Allah Aliyetakasika na kutukuka: Nimewaandalia…
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka amesema: Nimetayarisha na nimeandaa kwa ajili ya kuwatukuza waja wangu wema peponi mambo ambayo uhalisia wake hakuna jicho liliwahi kuona, na wala sikio lolote kusikia wasifu wake, wala kutokea wala kupita ndani ya moyo wa binadamu yeyote uhalisia wake. Akasema Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Someni mkitaka:
"Nafsi yoyote haijui yale waliyofichiwa miongoni mwa mambo yenye kutuliza macho" [As-Sajda: 17]
Mafunzo: Amesema Allah Aliyetakasika na kutukuka: Nimewaandalia…
- Hadithi hii ni katika zile anazozipokea Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Mola wake Mlezi, na huitwa Hadithil Qudsi au Hadithil Ilahi, nayo ni ile ambayo tamko lake na maana yake inatoka kwa Allah, isipokuwa haina upekee kama wa Qur'ani inaojipambanua nayo kwa vingine, kama kisomo chake kutumika katika ibada, na kuwa twahara kabla ya kusoma, na kuwashinda watu kwa changamoto zake, na mengineyo.
- Himizo la kufanya matendo ya utiifu na kuacha maovu; ili kufaulu kwa kuyapata yale aliyoyaandaa Mwenyezi Mungu kwa waja wake wema.
- Mwenyezi Mungu hakutuonyesha ndani ya kitabu chake wala mafundisho ya Mtume wake yote yaliyoko peponi, na kwamba ambayo hatujayafahamu ni makubwa kuliko tuliyoyafahamu.
- Kumebainishwa ukamilifu wa neema za peponi, na kwamba wakazi wake watapata katika mambo ya kufurahisha yasiyokuwa na tabu wala mawazo ya namna kupatikana kwake.
- Starehe za dunia ni zenye kuisha na Akhera ndio bora na yenye kubakia.
Makundi :
Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha
· Sifa za pepo na moto.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
أستغفر الله
Je demande pardon à Allah