Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Linganeni sawa katika sijida, na asikunjue mmoja wenu mikono yake kama anavyokunjua mbwa
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعن أَنَس بن مالك رضي الله عنه عَنْ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: «اعْتَدِلُوا في السجود، ولا يَبْسُطْ أحدكم ذِرَاعَيْهِ انْبِسَاطَ الكلب».
Ameamrisha Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- kulingana katika sijida, na hii nikuwa, ili mwenye kuswali awe na muonekano mzuri katika sijida, kiasi kwamba aweke viganja vyake katika ardhi, na anyanyue miundi yake na aiweke mbali na mbavu zake, kwasababu hali hii ndio anuani ya uchangamfu na hamu vinavyohitajika ndani ya swala, na ni kwasababu muonekano huu mzuri unaviwezesha viungo vya kusujudu vyote kuchukua nafasi yake katika ibada. Na akakatazwa kunyoosha mikono miwili katika sijida; kwasababu hii ni dalili ya uvivu na uchovu, na kuna kujifananisha na mbwa, nako nikujifananisha na kisichofaa.
Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Sala. · Fiq'hi na misingi yake. · Sifa za Swala.