Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mimi ndiye mtu niliyekaribu zaid…
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعن أَبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه: أنه كَانَ يُكَبِّرُ فِي كُلِّ صَلَاةٍ مِنَ الْمَكْتُوبَةِ وَغَيْرِهَا، فِي رَمَضَانَ وَغَيْرِهِ، فَيُكَبِّرُ حِينَ يَقُومُ، ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَرْكَعُ، ثُمَّ يَقُولُ: سَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَهُ، ثُمَّ يَقُولُ: رَبَّنَا وَلَكَ الْحَمْدُ، قَبْلَ أَنْ يَسْجُدَ، ثُمَّ يَقُولُ: اللهُ أَكْبَرُ حِينَ يَهْوِي سَاجِدًا، ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَرْفَعُ رَأْسَهُ مِنَ السُّجُودِ، ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَسْجُدُ، ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَرْفَعُ رَأْسَهُ مِنَ السُّجُودِ، ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَقُومُ مِنَ الْجُلُوسِ فِي الِاثْنَتَيْنِ، وَيَفْعَلُ ذَلِكَ فِي كُلِّ رَكْعَةٍ، حَتَّى يَفْرُغَ مِنَ الصَّلَاةِ، ثُمَّ يَقُولُ حِينَ يَنْصَرِفُ: وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، إِنِّي لَأَقْرَبُكُمْ شَبَهًا بِصَلَاةِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، إِنْ كَانَتْ هَذِهِ لَصَلَاتَهُ حَتَّى فَارَقَ الدُّنْيَا.
Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- anapokea sehemu katika sifa ya swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na anaeleza kuwa alipokuwa akisimama katika sala anatoa takbira wakati ananyanyuka, nayo ni takbira ya kuhirimia swala, kisha anatoa takbira wakati anahama kwenda katika rukuu, na wakati anasujudu, na wakati anaponyanyua kichwa chake kutoka katika sijida, na wakati anasujudu sijida ya pili, na anaponyanyua kichwa chake kutoka katika sijida hiyo, na anaponyanyuka katika rakaa mbili za mwanzo baada ya kikao cha tashahudi ya kwanza katika swala yenye rakaa tatu au nne, kisha anafanya hivyo katika swala nzima mpaka anamaliza, na alikuwa akisema anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuu: Sami'allaahu liman hamidah, kisha anasema akiwa wima: Rabbanaa lakal hamdu.
Kisha anasema Abuu Huraira wakati anapomaliza swala: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mimi swala yangu iko karibu zaidi kufanana na swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- zaidi yenu, bali hii ndio ilikuwa sifa ya sala yake mpaka alipoondoka duniani.
Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Sala. · Fiq'hi na misingi yake. · Sifa za Swala.