Atakayehifadhi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa nne baada yake basi Mwenyezi Mungu ata…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Atakayehifadhi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa nne baada yake basi Mwenyezi Mungu ata…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na Ahmad
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Atakayehifadhi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa nne…
Maelezo ya hadith: Atakayehifadhi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa nne…
Amempa habari njema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake atakayeswali katika swala za sunna rakaa nne kabla ya swala ya Adhuhuri, na rakaa nne baada yake, na akadumu na akazihifadhi, kuwa Mwenyezi Mungu atamharamisha kuingia motoni.
Mafunzo: Atakayehifadhi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa nne…
- Ni sunna kuhifadhi rakaa nne kabla ya Adhuhuri, na nne baada yake.
- Sunna zilizopangwa za kabla ya swala - Yaani kabla ya swala za faradhi-; zina hekima kubwa, miongoni mwake: Ni kumuandaa mwenye kuswali kwa ajili ya ibada kabla ya kuingia katika swala ya faradhi, na ama za baada ya swala miongoni mwa hekima zake ni kuziba mapungufu ya swala za faradhi.
- Sunna zilizopangiliwa zina faida kubwa, ikiwemo kuzidisha mema, na kufuta madhambi, na kunyanyua daraja.
- Kanuni ya Ahlussunna (wanaofuata mafundisho ya Mtume) katika hadithi za ahadi mfano wa hadithi hii: Ni kuchukuliwa kuwa, mpaka mtu afe katika hali ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu, nakuwa makusudio yake ni kutokaa milele motoni, kwa sababu mfanya madhambi ni katika watu wa tauhidi, anastahiki adhabu lakini hatowekwa motoni milele endapo ataadhibiwa.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Sala.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Swala ya Kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.
· Sunna za kila siku zilizopangiliwa
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
لا إله إلا الله
Pas de divinité sauf Allah