Msiwafanye Mayahudi na Manaswara kuwa ni wakweli wala ni waongo, na semeni hivi {Tumemuami…

Islam > Sw > Hadith > Quran tukufu na elimu zake > Msiwafanye Mayahudi na Manaswara kuwa ni wakweli wala ni waongo, na semeni hivi {Tumemuami…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Msiwafanye Mayahudi na Manaswara kuwa ni wakweli wala n…

عَنْ ‌أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: كَانَ أَهْلُ الْكِتَابِ يَقْرَؤُونَ التَّوْرَاةَ بِالْعِبْرَانِيَّةِ، وَيُفَسِّرُونَهَا بِالْعَرَبِيَّةِ لِأَهْلِ الْإِسْلَامِ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا تُصَدِّقُوا أَهْلَ الْكِتَابِ وَلَا تُكَذِّبُوهُمْ، وَقُولُوا: {آمَنَّا بِاللهِ وَمَا أُنْزِلَ إِلَيْنَا} [البقرة: 136] الْآيَةَ».

Maelezo ya hadith: Msiwafanye Mayahudi na Manaswara kuwa ni wakweli wala n…

Aliutahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Umma wake kutodanganyika kwa habari wanazozipokea Mayahudi na Manaswara kutoka kwenye vitabu vyao, Pindi walipokuwa Mayahudi katika zama za Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake- wakisoma Taurati kwa lugha ya Kiebrania, nayo ni lugha ya Mayahudi, na wakitafsiri kwa lugha ya Kiarabu, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Msiwafanye Mayahudi na Manaswara kuwa ni wakweli na wala msiwafanye kuwa ni waongo, na hivi ni kwa yale mambo ambayo hayajulikani ukweli wake wala

uongo wake; Na kufanya hivyo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuamrisha tuamini vilivyoteremshwa kwetu katika Qur'ani, na vilivyoteremshwa kwao katika kitabu, isipokuwa hatuna namna ya kujua usahihi uliokuwepo katika vitabu hivyo ili kuepukana na visivyokuwa sahihi, kwa kuwa haikupokelewa katika sheria zetu chenye kuweka wazi ukweli wake ulioepukana na uongo wake, Hivyo tunasimama, hatuwafanyi kuwa ni wa kweli tusijekuwa pamoja nao katika zile sheria walizozibadilisha kutoka katika kitabu hicho wala hatuwafanyi kuwa ni waongo; huenda likawa jambo ni sahihi, hivyo tukawa ni wenye kupinga kile alichotuamrisha tukiamini, Na ametuamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- tuseme: {Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale yote aliyoyateremsha kwetu sisi, na yaliyoteremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-haqa na As-baatwi, na aliyopewa Mussa na Issa na waliyopewa Manabii kutoka kwa Mola wao, hatutofautishi yeyote miongoni mwao na sisi kwake yeye tumejisalimisha} (Al-Baqara:136).

Mafunzo: Msiwafanye Mayahudi na Manaswara kuwa ni wakweli wala n…

Makundi : Qur'an tukufu na Elimu zake · Tafsiri ya Qur'an. · Rules and Principles of Exegesis · Akida- Itikadi- · Kuamini vitabu · Pre-Islamic Scriptures

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
لا إله إلا الله Pas de divinité sauf Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56