Mauti yataletwa yakiwa kama dume la Kondoo mwenye rangi mchanganyiko ya weusi na weupe

Islam > Sw > Hadith > Quran tukufu na elimu zake > Mauti yataletwa yakiwa kama dume la Kondoo mwenye rangi mchanganyiko ya weusi na weupe

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Mauti yataletwa yakiwa kama dume la Kondoo mwenye rangi…

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يُؤْتَى بِالْمَوْتِ كَهَيْئَةِ كَبْشٍ أَمْلَحَ، فَيُنَادِي مُنَادٍ: يَا أَهْلَ الجَنَّةِ، فَيَشْرَئِبُّونَ وَيَنْظُرُونَ، فَيَقُولُ: هَلْ تَعْرِفُونَ هَذَا؟ فَيَقُولُونَ: نَعَمْ، هَذَا المَوْتُ، وَكُلُّهُمْ قَدْ رَآهُ، ثُمَّ يُنَادِي: يَا أَهْلَ النَّارِ، فَيَشْرَئِبُّونَ وَيَنْظُرُونَ، فَيَقُولُ: وهَلْ تَعْرِفُونَ هَذَا؟ فَيَقُولُونَ: نَعَمْ، هَذَا المَوْتُ، وَكُلُّهُمْ قَدْ رَآهُ، فَيُذْبَحُ ثُمَّ يَقُولُ: يَا أَهْلَ الجَنَّةِ خُلُودٌ فَلاَ مَوْتَ، وَيَا أَهْلَ النَّارِ خُلُودٌ فَلاَ مَوْتَ، ثُمَّ قَرَأَ: {وَأَنْذِرْهُمْ يَوْمَ الحَسْرَةِ إِذْ قُضِيَ الأَمْرُ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ} [مريم: 39]، وَهَؤُلاَءِ فِي غَفْلَةٍ أَهْلُ الدُّنْيَا {وَهُمْ لاَ يُؤْمِنُونَ} [مريم: 39]».

Maelezo ya hadith: Mauti yataletwa yakiwa kama dume la Kondoo mwenye rangi…

Ameweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mauti yataletwa siku ya Kiyama, kwa mfano wa dume la kondoo lilochanganya rangi nyeupe na nyeusi, Basi ataita mwenye kuita: Enyi watu wa peponi! Basi watainua shingo zao na watainua vichwa vyao na wataangalia, Basi atawaambia: Je mnamjua huyu? Basi watasema: Ndiyo haya ni mauti, na wote kwa hakika wameyaona na kuyajua, Kisha muitaji ataita: Enyi watu wa Motoni, na watainua shingo zao na vichwa vyao na wataangalia, Basi atasema: Je mnamjua huyu? Hivyo watamjibu: Ndiyo, haya ni mauti, na wote wameyaona; Basi atachinjwa, kisha atasema mwenye kuita: Enyi watu wa peponi bakieni humo milele na hakuna kufa, na enyi watu wa Motoni bakieni humo milele na wala hakuna kufa, Na kumefanywa hivyo ili iwe ni ziada ya neema kwa waumini, na iwe ni adhabu yenye kuumiza kwa makafiri. Kisha akasoma Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake: "Na uwaonye siku ya majuto wakati hukumu ya kuingia peponi na motoni itakapotolewa, nao wapo kwenye kughafilika na wala hawaamini" Hivyo basi siku ya Kiyama watatenganishwa watu wa Peponi na watu wa Motoni, na wataingia wote kule walipopangiwa na kukaa humo milele, Basi atajuta mkosaji atapata mshituko na kujuta kwa nini hakufanya mema, na mwenye matendo machache pia kwa nini hakuzidisha mambo ya heri.

Mafunzo: Mauti yataletwa yakiwa kama dume la Kondoo mwenye rangi…

Makundi : Qur'an tukufu na Elimu zake · Tafsiri ya Qur'an. · Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Akida- Itikadi- · Sifa za pepo na moto. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima. · Kuamini siku ya mwisho · Tafsiri za Aya

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله Gloire à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56