“Ewe mwanadam, maadamu unaniomba na kunitumainia, nitakusamehe uliyo nayo wala sitojali

Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > “Ewe mwanadam, maadamu unaniomba na kunitumainia, nitakusamehe uliyo nayo wala sitojali

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Tirmidhiy

Ni nzuri (Hasan)

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: “Ewe mwanadam, maadamu unaniomba na kunitumainia, nitak…

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ فِيكَ وَلاَ أُبَالِي، يَا ابْنَ آدَمَ لَوْ بَلَغَتْ ذُنُوبُكَ عَنَانَ السَّمَاءِ ثُمَّ اسْتَغْفَرْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ، وَلاَ أُبَالِي، يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ لَوْ أَتَيْتَنِي بِقُرَابِ الأَرْضِ خَطَايَا ثُمَّ لَقِيتَنِي لاَ تُشْرِكُ بِي شَيْئًا لأَتَيْتُكَ بِقُرَابِهَا مَغْفِرَةً».

Maelezo ya hadith: “Ewe mwanadam, maadamu unaniomba na kunitumainia, nitak…

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Hadithil Qudsi (tukufu): Ewe mwanadam, madam unaniomba na kutaraji rehema yangu, wala hujakata tamaa; Nitayasitiri madhambi yako na kuyafuta, bila kujali, hata kama madhambi na maasi haya ni katika madhambi makubwa. Ewe mwanadam! Lau madhambi yako yangekuwa mengi sana kiasi cha kuijaza nafasi ya baina ya mbingu na ardhi mpaka kiasi cha kufikia upenyo wake na kufunika pembe zake, kisha ukaniomba msamaha, basi ningekufutia na kukusamehe madhambi yote, bila kujali wingi wake.

Ewe mwanadam: Lau ungenijia mimi baada ya kufa ukiwa na madhambi na maasi ujazo wa ardhi, na ukafa haliyakuwa unanipwekesha hukunishirikisha na chochote; Ningekutana na madhambi na maasi haya nikiijaza ardhi kwa msamaha; kwa sababu mimi ni mwingi wa msamaha, na ninasamehe madhambi yote isipokuwa shirki.

Mafunzo: “Ewe mwanadam, maadamu unaniomba na kunitumainia, nitak…

Makundi : Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Akida- Itikadi- · Toba · Mambo mazuri na Adabu- Heshima. · Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka · Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
الله أكبر Allah est le plus grand

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56