Islam > Sw > Hadith > Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha > Wakati wakazi wa Peponi watakapoingia Peponi, Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, at…
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa watakapoingia watu wa peponi peponi, Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka atasema kuwaambia:
Je, mnahitaji chochote nikuongezeeni?
Watasema watu wa peponi wote kwa pamoja: Kwani hujazitia nuru nyuso zetu, kwani hujatuingiza peponi, na ukatuokoa na moto?
Hapo, Mwenyezi Mungu Mtukufu ataondoa pazia na kulinyanyua; na pazia lake ni nuru, watajikuta hawajapewa kitu wanachokipenda zaidi kwao kuliko kumtazama Mola wao Mlezi Aliyetakasika na kutukuka.
Makundi : Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Sifa za pepo na moto. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.