Mtakapo vaa, na mtakapo tawadha, basi anzeni na kuliani kwenu

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Mtakapo vaa, na mtakapo tawadha, basi anzeni na kuliani kwenu

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na Ahmad

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Mtakapo vaa, na mtakapo tawadha, basi anzeni na kuliani…

عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعًا: «إِذَا لَبِسْتُم، وَإِذَا تَوَضَّأتُم، فَابْدَأُوا بَأَيَامِنُكُم».

Maelezo ya hadith: Mtakapo vaa, na mtakapo tawadha, basi anzeni na kuliani…

Imetilia mkazo hadithi ya Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake swala la kuanza na kulia katika mambo mazuri, ikapokelewa kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Mtakapo vaa" Yaani mkitaka kuvaa. "Na mtakapo tawadha" Yaani mkitaka kufanya. "Anzeni na kuliani kwenu" ni wingi wa kulia nacho ni kinyume cha kushoto, aingize upande wa kulia wa kanzu, kabla ya kushoto na atangulize kulia katika mikono yake na miguu yake katika udhu, kisha tambua kuwa katika viungo vya udhu vipo ambavyo si sunna kuanza na kulia, navyo ni masikio mawili na viganja viwili na mashavu mawili, bali husafishwa vyote kwa wakati mmoja, ikiwa litakuwa gumu hilo kama ilivyo kwa aliyekatwa mkono na mfano wake atatanguliza kulia.

Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Twahara - usafi- · Adabu za kisheria. · Adabu za kuvaa. · Fiq'hi na misingi yake. · Udhu - kutawadha. · Sunna na Adabu za Kutawadha · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله Gloire à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56