Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapotengukwa udhu mpaka atawadhe
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapotengukwa udhu mpaka atawadhe
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapoten…
Maelezo ya hadith: Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapoten…
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa miongoni mwa sharti za kusihi swala: Ni twahara, ni wajibu kwa atakayetaka kuswali atawadhe ikiwa kimetokea kwake kitenguzi cha udhu; kama haja kubwa au ndogo au usingizi au kinginecho.
Mafunzo: Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapoten…
- Swala ya mtu mwenye hadathi (kama janaba, hedhi au nifasi) haikubaliki mpaka ajitwaharishe kwa kuoga kutokana na hadathi kubwa, na kwa kutawadha ikiwa ni hadathi ndogo (kama kwenda haja kubwa au ndogo, au kulala, au kutokwa upepo)
- Udhu ni kuchukua maji na kuyazungusha mdomoni na kuyatoa, kisha kuvuta maji kwa pumzi mpaka ndani ya pua, kisha kuyatoa na kuyapenga, kisha mtu ataosha uso wake mara tatu, kisha ataosha mikono yake pamoja viwiko viwili mara tatu, kisha atafuta kichwa chake mara moja, kisha kuosha miguu yake pamoja na fundo mbili mara tatu.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Twahara - usafi-
· Fiq'hi na misingi yake.
· Udhu - kutawadha.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
سبحان الله
Gloire à Allah