Yakwamba mtu mmoja alitawadha, akaacha sehemu ndogo saizi ya kucha miguuni kwake, akaiona …
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Yakwamba mtu mmoja alitawadha, akaacha sehemu ndogo saizi ya kucha miguuni kwake, akaiona …
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim
Ni sahihi kwa ushahidi wake mbalimbali
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Yakwamba mtu mmoja alitawadha, akaacha sehemu ndogo sai…
عَنْ جَابِرٍ رضي الله عنه قال: أَخْبَرَنِي عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ: أَنَّ رَجُلًا تَوَضَّأَ فَتَرَكَ مَوْضِعَ ظُفُرٍ عَلَى قَدَمِهِ فَأَبْصَرَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: «ارْجِعْ فَأَحْسِنْ وُضُوءَكَ» فَرَجَعَ، ثُمَّ صَلَّى.
Maelezo ya hadith: Yakwamba mtu mmoja alitawadha, akaacha sehemu ndogo sai…
Ameeleza Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimuona mtu mmoja kamaliza kutia udhu wake, akaacha kiasi cha kucha moja katika kisigino chake, hakikupatwa na maji ya udhu, akasema kumwambia huku akiashiria sehemu palipo na mapungufu: Rudi katie vizuri udhu wako, na utimize na ukipe kila kiungo haki yake katika maji, yule bwana akarudi akatimiza udhu wake kisha akaswali.
Mafunzo: Yakwamba mtu mmoja alitawadha, akaacha sehemu ndogo sai…
- Uwajibu wa kufanya haraka kuamrisha mema na kukataza maovu, na kumuelekeza asiyejua na aliyeghafilika, na hasa hasa uovu ukiwa unaambatana na kuharibika kwa ibada yake.
- Ulazima wa kueneza maji katika viungo vyote vya udhu, nakuwa mwenye kuacha sehemu ya kiungo -hata kama ni kidogo- udhu wake hautasihi, na itamlazimu kurudia ikiwa umepita muda mrefu tangu kumaliza udhu wake.
- Sheria ya kupendezesha udhu, na hii ni kwa kuutimiza na kueneza vizuri kwa namna iliyoamrishwa kisheria.
- Miguu miwili ni katika viungo vya udhu, na haitoshi kuifuta, bali ni lazima kuiosha.
- Ni lazima kufuatanisha baina ya viungo vya udhu, kiasi kwamba aoshe kila kiungo kabla hakijakauka kilicho kabla yake.
- Kutojua na kusahau havidondoshi wajibu, bali vinadondosha dhambi, huyu bwana ambaye hakutimiza udhu wake kwa sababu ya kutojua kwake, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hakumdondoshea uwajibu, ambao ni udhu, bali alimuamrisha kurudia.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Twahara - usafi-
· Fiq'hi na misingi yake.
· Udhu - kutawadha.
· Nguzo za Udhu.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
اللهم صل على محمد
Ô Allah prie sur Muhammad