Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Atayeapa kinyume na Mwenyezi Mungu basi atakuwa amekufuru au kafanya ushirikina
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعن ابْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما أنه سَمِعَ رَجُلًا يَقُولُ: لَا وَالْكَعْبَةِ، فَقَالَ ابْنُ عُمَرَ: لَا يُحْلَفُ بِغَيْرِ اللَّهِ، فَإِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «مَنْ حَلَفَ بِغَيْرِ اللهِ فَقَدْ كَفَرَ أَوْ أَشْرَكَ».
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu na majina yake na sifa zake basi atakuwa kamkufuru Mwenyezi Mungu au kafanya ushirikina; kwa sababu kiapo humaanisha kutukuzwa mwenye kuapiwa, na utukufu ni wa Allah pekee; hakuapiwi ila kwa Allah na majina yake na sifa zake kutakasika machafu ni kwake. Na kiapo hiki ni katika shirki ndogo; lakini ikiwa muapaji atakitukuza alichokiapia kama anavyomtukuza Allah Mtukufu au zaidi; basi hapo itakuwa katika ushirikina mkubwa.
Makundi : Akida- Itikadi- · Majina na Hukumu. · Ushirikina.