Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Nilimuendea Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, …
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعن أبي ثَعْلبة الخُشني رضي الله عنه قال: «أَتَيْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم فقلت: يا رسول الله، إنا بأرض قوم أهل كتاب، أَفَنَأْكُلُ في آنِيَتِهِم؟ وفي أرض صيد، أَصِيدُ بِقَوْسِي وبِكَلْبِي الذي ليس بِمُعَلَّمٍ، وبِكَلْبِي المُعَلَّمِ، فما يَصلح لي؟ قال: أمَّا مَا ذَكَرْتَ- يعني من آنية أهل الكتاب-: فإِنْ وجدْتُمْ غيرها فلا تأكلوا فيها، وإِنْ لم تَجِدُوا فاغسِلوهَا، وكلوا فِيهَا، وما صدتَ بِقَوْسِكَ، فذَكَرْتَ اسمَ الله عَلَيه فَكُلْ، وما صِدْتَ بِكَلْبِكَ المُعَلَّمِ، فَذَكَرْتَ اسْمَ الله عليه فَكُلْ، وما صِدْتَ بِكَلْبِكَ غيرِ المُعَلَّمِ فَأَدْرَكْتَ ذَكَاتَهُ فَكُلْ».
Alieleza Abuu Thaalaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakuwa wao wamepewa mtihani wa ujirani wa watu wa kitabu, na makusudio ya hao ni mayahudi na wakristo, je ni halali kwao wale katika vyombo vyao pamoja na dhana ya unajisi wake? Akamjibu kuwa inafaa kula ndani yake, Na ni bora zaidi kuvitumia katika matumizi yasiyokuwa kula kwa sharti mbili: 1- Kutopatikana vyombo vingine tofauti na hivyo. 2- Na wavioshe. Na akamueleza kuwa wao wako katika ardhi ya mawindo, nakuwa yeye anawinda kwa upinde wake na kwa mbwa wake aliyefunzwa juu ya uwindaji na adabu zake, na kwa mbwa wake ambaye hajafunzwa, ni kipi kinachofaa kwake na cha halali katika viwindwa vya hivi vifaa? Akamjibu kuwa alivyoviwinda kwa upinde wake basi hivyo ni halali, kwa sharti ataje jina la Mwenyezi Mungu -Mtukufu- wakati wa kurusha mshale. Na ama unavyoviwinda kwa mbwa, wakiwa wamefunzwa na ukataja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kumtuma hicho ni halali pia, na ama ambao hawajafunzwa, si halali viwindwa vyake isipokuwa atakapokikuta mtu kikiwa hai na akichinje kichinjo cha kisheria.
Makundi : Vyakula na vinywaji. · Hukumu za Vyakula na Vinywaji. · Uwindaji · Fiq'hi na misingi yake.