Wallahi – akipenda Mwenyezi Mungu - sitokula kiapo cha jambo fulani isipokuwa ninapoona ki…

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa miamala > Wallahi – akipenda Mwenyezi Mungu - sitokula kiapo cha jambo fulani isipokuwa ninapoona ki…

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Wallahi – akipenda Mwenyezi Mungu - sitokula kiapo cha…

Maelezo ya hadith: Wallahi – akipenda Mwenyezi Mungu - sitokula kiapo cha…

Anasimulia Abuu Musa Al-Ash’ari radhi za Allah ziwe juu yake kuwa, alikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akiwa na kundi la kabila lake, na makusudio yao yalikuwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, ili awape ngamia wapande, ili kuweza kushiriki katika jihadi, aliapa rehema na amani ziwe juu yake kuwa hatowabeba, na hakuwa hana chochote cha kuwabeba, basi wakarudi na kukaa kwa muda, kisha wakaletewa ngamia watatu kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawatumia wale mabwana, baadhi yao wakaambiana: Mwenyezi Mungu asitubariki kwa ngamia hawa; Kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliapa kutotubeba, basi wakamjia na wakamuuliza, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Aliyekubebeni ni Mwenyezi Mungu Mtukufu; Kwa sababu yeye ndiye aliyetoa ufanikishaji na akaruzuku, lakini mimi ni sababu ya haya kutokea kupitia mikono yangu, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Wallahi, akipenda Mwenyezi Mungu, sitaapa kufanya au kuacha chochote, na nikaona kuwa kisichokuwa kiapo hicho ni heri na bora zaidi, isipokuwa nitafanya lililo bora zaidi, na kuyaacha niliyoapa, na ninalipa kafara ya kiapo changu.

Mafunzo: Wallahi – akipenda Mwenyezi Mungu - sitokula kiapo cha…

Makundi : Fiq'hi - Ufahamu- wa miamala. · Viapo na Nadhiri. · Fiq'hi na misingi yake.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
أستغفر الله Je demande pardon à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56