Atakayechukua elimu katika elimu ya unajimu basi atakuwa kajichukulia sehemu ya uchawi, at…
Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Atakayechukua elimu katika elimu ya unajimu basi atakuwa kajichukulia sehemu ya uchawi, at…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Atakayechukua elimu katika elimu ya unajimu basi atakuw…
عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «من اقتبَسَ علْمًا مِنَ النُّجُومِ اقْتبَسَ شُعبَة مِن السِّحرِ، زادَ ما زادَ».
Maelezo ya hadith: Atakayechukua elimu katika elimu ya unajimu basi atakuw…
Anaeleza Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- yakuwa atakayejifunza na akachukua katika elimu ya nyota na mashukio yake na kutumia harakati zake kama ushahidi wa matukio ya ardhini kama kifo cha mtu fulani au uhai wake au maradhi yake, na mfano wake katika yatakayotokea siku za mbeleni, basi atakuwa kajifunza sehemu ya uchwi, nakuwa kadiri mwanadamu anavyokithirisha elimu hii basi anakithirisha uchawi.
Mafunzo: Atakayechukua elimu katika elimu ya unajimu basi atakuw…
- Uharamu wa unajimu ambao ni kueleza mambo yajayo kwa kutegemea hali za nyota; hili kwa sababu ni katika kudai elimu ya ghaibu.
- Kwa hakika unajimu ulioharamishwa ni katika aina za uchwi zinazopingana na tahuhidi, tofauti na kuzitazama nyota kwa ajili ya kujua uelekeo au kibla au kuingia kwa msimu na miezi haya ni halali.
- Kila anavozidisha katika kujifunza ndivyo anavyozidi kujifunza sehemu ya uchawi.
- Nyota zinafaida tatu amezitaja Mwenyezi Mungu ndani ya kitabu chake: Ni pambo la mbingu, na ni alama hutumika kuongozea, na kipigo kwa mashetani
Makundi :
Akida- Itikadi-
· Majina na Hukumu.
· Vitenguzi vya uislamu.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
أستغفر الله
Je demande pardon à Allah