Hakuna siku ambayo wanaamka ndani yake waja isipokuwa kuna Malaika wawili wanateremka, ana…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Hakuna siku ambayo wanaamka ndani yake waja isipokuwa kuna Malaika wawili wanateremka, ana…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Hakuna siku ambayo wanaamka ndani yake waja isipokuwa k…
Maelezo ya hadith: Hakuna siku ambayo wanaamka ndani yake waja isipokuwa k…
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa katika kila siku inayochomozewa na Jua ndani yake kuna Malaika wawili wanateremka na kunadi, anasema mmoja wao:
Ewe Mwenyezi Mungu mpe mwenye kutoa katika njia za utiifu na kwa familia na kwa wageni na sadaka za hiyari mrejeshee na mpe badala bora kuliko kile alichotoa, na umbariki.
Na anasema mwingine: Ewe Mwenyezi Mungu mpe bahili mzuiaji uharibifu katika mali yake na uiteketeze mali yake anayoizuia na kutompa mwenye kustahiki.
Mafunzo: Hakuna siku ambayo wanaamka ndani yake waja isipokuwa k…
- Inafaa kumuombea dua nzuri mkarimu kuzidishiwa badala, na kurejeshewa kheri zaidi ya ile aliyotoa, na inafaa kumuombea dua mbaya bahili kwa kuharibika mali yake ambayo anaifanyia ubahili na anaizuia kuitoa katika yale aliyowajibishiwa na Mwenyezi Mungu juu yake.
- Dua ya Malaika kuwaombea waumini wema wenye kutoa, kuwaombea kheri na baraka, nakuwa dua zao hujibiwa.
- Himizo la kutoa katika yale ya wajibu na ya hiyari; kama kutoa matumizi kwa familia, na kuunga udugu, na milango mbali mbali ya kheri.
- Kumebainishwa fadhila za mtoaji katika njia za kheri, nakuwa mwisho wake nikuwa Mwenyezi Mungu humrejeshea badala, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na wala hamtatoa chochote ila yeye atakirejesha, naye ni mbora wa wanaoruzuku" [Sabai:39].
- Dua hii mbaya ni kwa mtu bahili katika matumizi ya wajibu, ama matumizi ya hiyari dua haingii hapo; kwa sababu mwenye mali hapa hastahiki dua hii.
- Uharamu wa ubahili na tamaa.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Zaka.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Sadaka za kujitolea.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
لا حول ولا قوة إلا بالله
Pas de force ni de puissance sauf en Allah