Tulikuwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake,inakaribia kama watu tisa au nane au saba…

Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Tulikuwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake,inakaribia kama watu tisa au nane au saba…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Tulikuwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake,inakar…

عَنْ أَبِي مُسْلِمٍ الْخَوْلَانِيِّ، قَالَ: حَدَّثَنِي الْحَبِيبُ الْأَمِينُ، أَمَّا هُوَ فَحَبِيبٌ إِلَيَّ، وَأَمَّا هُوَ عِنْدِي فَأَمِينٌ، عَوْفُ بْنُ مَالِكٍ الْأَشْجَعِيُّ رضي الله عنه قَالَ: كُنَّا عِنْدَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، تِسْعَةً أَوْ ثَمَانِيَةً أَوْ سَبْعَةً، فَقَالَ: «أَلَا تُبَايِعُونَ رَسُولَ اللهِ؟» وَكُنَّا حَدِيثَ عَهْدٍ بِبَيْعَةٍ، فَقُلْنَا: قَدْ بَايَعْنَاكَ يَا رَسُولَ اللهِ، ثُمَّ قَالَ: «أَلَا تُبَايِعُونَ رَسُولَ اللهِ؟» فَقُلْنَا: قَدْ بَايَعْنَاكَ يَا رَسُولَ اللهِ، ثُمَّ قَالَ: «أَلَا تُبَايِعُونَ رَسُولَ اللهِ؟» قَالَ: فَبَسَطْنَا أَيْدِيَنَا وَقُلْنَا: قَدْ بَايَعْنَاكَ يَا رَسُولَ اللهِ، فَعَلَامَ نُبَايِعُكَ؟ قَالَ: «عَلَى أَنْ تَعْبُدُوا اللهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا، وَالصَّلَوَاتِ الْخَمْسِ، وَتُطِيعُوا -وَأَسَرَّ كَلِمَةً خَفِيَّةً- وَلَا تَسْأَلُوا النَّاسَ شَيْئًا» فَلَقَدْ رَأَيْتُ بَعْضَ أُولَئِكَ النَّفَرِ يَسْقُطُ سَوْطُ أَحَدِهِمْ، فَمَا يَسْأَلُ أَحَدًا يُنَاوِلُهُ إِيَّاهُ.

Maelezo ya hadith: Tulikuwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake,inakar…

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kundi la Masahaba, akawataka mara tatu mfululizo wampe ahadi ya utiifu na wampe ahadi ya kushikamana na mambo haya:

La kwanza: Kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake kwa kutekeleza amri zake na kujiepusha na makatazo yake, na wasimshirikishe na kitu kingine.

La pili: Kusimamisha swala tano za faradhi, katika usiku na mchana.

La tatu: Kusikia na kutii katika mambo mema kwa yule atakayesimamia majukumu ya waislamu.

La nne: Kushusha haja zao zote kwa Mwenyezi Mungu na wasiwaombe watu chochote katika haja hizo, na katika hilo Mtume rehema na amani ziwe juu yake akashusha sauti yake.

Na hakika Masahaba radhi za Allah ziwe juu yao waliyafanyia kazi yale waliyoyatolea ahadi, mpaka akasema mpokezi wa hadithi: Hakika niliwaona baadhi yao hao Masahaba unadondoka mjeledi wa mmoja wao, na hamuombi yeyote amuokotee, bali anashuka na anauchukua yeye mwenyewe.

Mafunzo: Tulikuwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake,inakar…

Makundi : Akida- Itikadi- · Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka · Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.

بسم الله الرحمن الرحيم mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
أحدب متناقص Gibbeuse Décroissante Jour 16.7 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
لا إله إلا الله Pas de divinité sauf Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56