Atakayepatwa na umasikini akaushusha kwa watu hautozibwa umasikini wake, na atakayeushusha…

Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Atakayepatwa na umasikini akaushusha kwa watu hautozibwa umasikini wake, na atakayeushusha…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na Ahmad

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Atakayepatwa na umasikini akaushusha kwa watu hautozibw…

عن ابن مسعود رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «من أصابته فَاقَة فأنْزَلها بالناس لم تُسَدَّ فَاقَتُهُ، ومن أنْزَلها بالله، فَيُوشِكُ الله له بِرزق عاجل أو آجل».

Maelezo ya hadith: Atakayepatwa na umasikini akaushusha kwa watu hautozibw…

Ameeleza bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayepatwa na umasikini" Yaani: shida kubwa, na yamekithiri matumizi ya neno hili katika umasikini na maisha magumu. "Akauteremsha kwa watu" Yaani: Aliweka wazi kwao, na akaidhihirisha kwa njia ya malalamiko kwao, na akataka kuondolewa kwa umasikini wake toka kwao. Hivyo matokeo ni: "Hautozibwa umasikini wake" Yaani: haitokidhiwa haja yake, na hautoondoka umasikini wake, kila inapotatuliwa shida yake inampata shida nyingine zaidi ya hiyo. Na ama "atakayeishusha kwa Mwenyezi Mungu" akategemea kwa Mola wake basi "anakuwa karibu mno Mwenyezi Mungu" Kumpa haraka "kwake riziki ya haraka, yuko karibu kumpa mali na amfanye kuwa tajiri "Au ya baadaye" katika Akhera.

Makundi : Akida- Itikadi- · Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka · Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله Gloire à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56