kanipinga mwanadamu na hakustahiki kufanya hivyo, na amenitukana na hakustahiki kufanya hi…

Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > kanipinga mwanadamu na hakustahiki kufanya hivyo, na amenitukana na hakustahiki kufanya hi…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: kanipinga mwanadamu na hakustahiki kufanya hivyo, na am…

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «قَالَ اللَّهُ: كَذَّبَنِي ابْنُ آدَمَ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ، وَشَتَمَنِي وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ، فَأَمَّا تَكْذِيبُهُ إِيَّايَ فَقَوْلُهُ: لَنْ يُعِيدَنِي، كَمَا بَدَأَنِي، وَلَيْسَ أَوَّلُ الخَلْقِ بِأَهْوَنَ عَلَيَّ مِنْ إِعَادَتِهِ، وَأَمَّا شَتْمُهُ إِيَّايَ فَقَوْلُهُ: اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا وَأَنَا الأَحَدُ الصَّمَدُ، لَمْ أَلِدْ وَلَمْ أُولَدْ، وَلَمْ يَكُنْ لِي كُفْؤًا أَحَدٌ».

Maelezo ya hadith: kanipinga mwanadamu na hakustahiki kufanya hivyo, na am…

Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika hadithil Qudsi yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ameeleza kuhusu washirikina na makafiri kuwa wao humkanusha na humsifu kwa sifa za mapungufu na za aibu, na hawakutakiwa kufanya hivyo.

Ama kumkanusha kwao Mwenyezi Mungu: Ni kudai kwao kuwa Mwenyezi Mungu hatowarejesha kwa mara nyingine baada ya kufa kwao kama alivyowaumba mara ya kwanza kutoka katika kutokuwepo, akawajibu kuwa aliyeanza kuumba mwanzo anauwezo wa kuwarudisha, bali hilo ni jepesi mno, japo kuwa uhalisia kwa Mwenyezi Mungu yote ni mepesi, kuumba kwanzia mwanzo na kurudisha, kwani Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu ni muweza.

Na ama kutukana kwao: Ni kauli yao: Kuwa yeye ana mtoto, akawajibu kuwa yeye ni wa pekee aliyepwekeka kwa ukamilifu wote katika majina yake na sifa zake na vitendo vyake, aliyetakasika na kila mapungufu na aibu, wa pekee asiyehitaji kwa yeyote, na anahitaji kwake kila mmoja, na hakuwahi kuwa mzazi wa yeyote, na hakuwahi kuwa mtoto wa yeyote, na hakuna yeyote anayefanana naye hata mmoja kwa kuwa na mfanano au mwendano, ametakasika na kutukuka.

Mafunzo: kanipinga mwanadamu na hakustahiki kufanya hivyo, na am…

Makundi : Akida- Itikadi- · Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka · Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
لا حول ولا قوة إلا بالله Pas de force ni de puissance sauf en Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56