Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi nitakuwa nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu…

Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi nitakuwa nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi nitakuwa nimem…

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ اللَّهَ قَالَ: مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالحَرْبِ، وَمَا تَقَرَّبَ إِلَيَّ عَبْدِي بِشَيْءٍ أَحَبَّ إِلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُ عَلَيْهِ، وَمَا يَزَالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إِلَيَّ بِالنَّوَافِلِ حَتَّى أُحِبَّهُ، فَإِذَا أَحْبَبْتُهُ: كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بِهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بِهِ، وَيَدَهُ الَّتِي يَبْطِشُ بِهَا، وَرِجْلَهُ الَّتِي يَمْشِي بِهَا، وَإِنْ سَأَلَنِي لَأُعْطِيَنَّهُ، وَلَئِنِ اسْتَعَاذَنِي لَأُعِيذَنَّهُ، وَمَا تَرَدَّدْتُ عَنْ شَيْءٍ أَنَا فَاعِلُهُ تَرَدُّدِي عَنْ نَفْسِ المُؤْمِنِ، يَكْرَهُ المَوْتَ وَأَنَا أَكْرَهُ مَسَاءَتَهُ».

Maelezo ya hadith: Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi nitakuwa nimem…

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika hadithil Qudsi yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Atakayemuudhi kipenzi miongoni mwa vipenzi vyangu na akamkasirisha na akambughudhi basi nitakuwa nimemtangazia uadui.

Na walii (Kipenzi) ni: Muumini mchamungu, na kwa kadiri imani na uchamungu wa mja unavyokuwa ndivyo nafasi yake ya ukaribu inavyokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Na hajawahi muislamu kujiweka karibu kwa Mola wake kwa jambo alipendalo zaidi kuliko lile alilomfaradhishia na akamuwajibishia juu yake, ikiwemo kufanya mambo yote ya utiifu, na kuacha maharamisho, na kwa kadiri anavyoendelea muislamu kujikurubisha kwa Mola wake kwa yale ya sunna pamoja na faradhi; mpaka atapata mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu akimpenda, atakuwa akimtimizia mambo yake katika viungo hivi vinne:

Atampa umakini katika kusikia kwake, hatosikia ila yale yenye kumridhisha Mwenyezi Mungu.

Na humpa umakinifu katika macho yake, hatotazama ila yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu kuyatazama na anayaridhia.

Na anampa umakinifu katika mkono wake, hatofanya kwa mkono wake ila yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu.

Na anampa umakinifu katika mguu wake, hatokwenda ila katika yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu, na wala hatoyaendea ila yale yenye kheri ndani yake.

Pamoja na haya yote, akimuomba Mwenyezi Mungu chochote basi Mwenyezi Mungu humpa alichoomba, anakuwa ni mtu mwenye kujibiwa maombi, na ikiwa atataka hifadhi kwa Mwenyezi Mungu na akaomba ulinzi kwake kwa kutaka hifadhi, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu humkinga dhidi ya yale anayoyahofu.

Kisha akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na sijawahi kusita katika jambo ninalotaka kulifanya kama kusita kwangu katika kuichukua nafsi ya muumini, kwa kumhurumia; kwa sababu yeye anachukia kifo kwa kuwa ndani yake kuna maumivu, na Mwenyezi Mungu hapendi yanayomuudhi muumini.

Mafunzo: Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi nitakuwa nimem…

Makundi : Akida- Itikadi- · Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka · Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله وبحمده Gloire et louange à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56