Namuapa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, kwa hakika vyombo vyake ni vingi kama …

Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Namuapa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, kwa hakika vyombo vyake ni vingi kama …

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Namuapa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, kwa…

عَنْ أَبِي ذَرٍّ رضي الله عنه قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ مَا آنِيَةُ الْحَوْضِ؟ قَالَ: «وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لَآنِيَتُهُ أَكْثَرُ مِنْ عَدَدِ نُجُومِ السَّمَاءِ وَكَوَاكِبِهَا، أَلَا فِي اللَّيْلَةِ الْمُظْلِمَةِ الْمُصْحِيَةِ، آنِيَةُ الْجَنَّةِ مَنْ شَرِبَ مِنْهَا لَمْ يَظْمَأْ آخِرَ مَا عَلَيْهِ، يَشْخَبُ فِيهِ مِيزَابَانِ مِنَ الْجَنَّةِ، مَنْ شَرِبَ مِنْهُ لَمْ يَظْمَأْ، عَرْضُهُ مِثْلُ طُولِهِ، مَا بَيْنَ عَمَّانَ إِلَى أَيْلَةَ، مَاؤُهُ أَشَدُّ بَيَاضًا مِنَ اللَّبَنِ، وَأَحْلَى مِنَ الْعَسَلِ».

Maelezo ya hadith: Namuapa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, kwa…

Ame apa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ya kuwa vyombo vya Birika lake siku ya kiyama, ni vingi kuliko nyota angani, na kuliko sayari za mbinguni, Na hilo litadhihiri katika usiku wenye kiza ambao hauna mwezi, kwa sababu usiku wenye kuangaza huwa hakuna ndani yake nyota zenye kuonekana kwa kujificha kwake kutokana na mwanga wa mwezi, ambao hauna mawingu, kwa sababu kuwepo kwa mawingu kunazuia kuonekana kwa nyota, Na kwa hakika vyombo vya peponi atakaye kunywa miongoni mwa vinywaji vilivyomo humo, inakuwa ndiyo mwisho kabisa kwa mnywaji kupata kinywaji kwa sababu ya kiu, Na Birika lake linachuruzisha kupitia mabomba mawili yatokayo peponi, na upana wake ni sawa na urefu wake; Hivyo Birika nguzo zake zote zipo sawa, urefu wake ni sawa na umbali ambao upo kati ya Amman mji ambao upo Sham mpaka Aila nao ni mji maarufu uliopo pembeni mwa mji wa Sham, Na maji ya Birika ni meupe sana kuliko maziwa, na ladha yake ni tamu zaidi kuliko Asali.

Mafunzo: Namuapa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, kwa…

Makundi : Akida- Itikadi- · Kuamini siku ya mwisho

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
لا إله إلا الله Pas de divinité sauf Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56