Kwa hakika Mwenyezi Mungu atamchagua mtu mmoja katika umma wangu mbele ya mkusanyiko wa wa…

Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Kwa hakika Mwenyezi Mungu atamchagua mtu mmoja katika umma wangu mbele ya mkusanyiko wa wa…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Tirmidhi na bin Majah

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Kwa hakika Mwenyezi Mungu atamchagua mtu mmoja katika u…

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ العَاصِ رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ اللهَ سَيُخَلِّصُ رَجُلًا مِنْ أُمَّتِي عَلَى رُءُوسِ الْخَلَائِقِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، فَيَنْشُرُ عَلَيْهِ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ سِجِلًّا، كُلُّ سِجِلٍّ مِثْلُ مَدِّ الْبَصَرِ، ثُمَّ يَقُولُ: أَتُنْكِرُ مِنْ هَذَا شَيْئًا؟ أَظَلَمَكَ كَتَبَتِي الْحَافِظُونَ؟ فَيَقُولُ: لَا يَا رَبِّ، فَيَقُولُ: أَفَلَكَ عُذْرٌ؟ فَيَقُولُ: لَا يَا رَبِّ، فَيَقُولُ: بَلَى إِنَّ لَكَ عِنْدَنَا حَسَنَةً، فَإِنَّهُ لَا ظُلْمَ عَلَيْكَ الْيَوْمَ، فَتُخْرَجُ بِطَاقَةٌ فِيهَا: أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، فَيَقُولُ: احْضُرْ وَزْنَكَ، فَيَقُولُ: يَا رَبِّ مَا هَذِهِ الْبِطَاقَةُ مَعَ هَذِهِ السِّجِلَّاتِ؟ فَقَالَ: إِنَّكَ لَا تُظْلَمُ، قَالَ: فَتُوضَعُ السِّجِلَّاتُ فِي كِفَّةٍ، وَالْبِطَاقَةُ فِي كِفَّةٍ، فَطَاشَتِ السِّجِلَّاتُ، وَثَقُلَتِ الْبِطَاقَةُ، فَلَا يَثْقُلُ مَعَ اسْمِ اللهِ شَيْءٌ».

Maelezo ya hadith: Kwa hakika Mwenyezi Mungu atamchagua mtu mmoja katika u…

Alitoa habari Mtume -Rehema na mani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu atamchagua mtu katika umma wake kwenye kundi la watu siku ya Kiyama atamuita ili amuhesabu, basi atamtolea mafaili tisini na tisa na mafaili hayo ni ya matendo yake mabaya ambayo alikuwa akiyafanya Duniani, na urefu wa kila faili ni mfano wa upeo wa macho, Kisha Mwenyezi Mungu atamwambia mtu huyu: Je unapinga chochote katika haya yaliyoandikwa katika mafaili? Je Malaika wangu wenye kuhifadhi wanayoandika wamekudhulumu? Basi atasema mtu yule: Hapana ewe Mola wangu. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atasema: Je una chochote cha kujitetea nacho katika matendo yako uliyoyatanguliza miongoni mwa matendo ya Duniani?katika matendo uliyoyafanya kwa kusahau au kwa kukosea au kwa kutojua, Basi atasema mtu yule: Hapana ewe Mola wangu sina chochote cha kujitetea nacho. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atasema: Si hivyo, kwa hakika wewe una mambo yaliyoandikwa kwetu sisi, na kwa hakika wewe hutodhulumiwa leo hii. Akasema: Basi itatolewa kadi iliyoandikwa ndani yake: Ash-hadu An-laa ilaaha illa llaah wa Ash-hadu Anna Muhammadan Ab-duhuu wa Rasuuluhu. Basi atasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Angalia Mizani yako. Basi atasema mtu yule hali ya kuona ajabu: Ewe Mola wangu! ni uzito wanini huu wa kikadi kidogo pamoja na kupimwa na mafaili yote haya? Basi atasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: hautadhulumiwa leo hii. Akasema: Basi mafaili yatawekwa katika sehemu ya kupimia, na Kadi kwenye sehemu nyingine ya kupimia; Hivyo basi ukawa mwepesi upande wa kupimia palipo na Mafaili na ukawa mzito upande wa kupimia palipo na Kadi, hivyo basi Mwenyezi Mungu akamsamehe.

Mafunzo: Kwa hakika Mwenyezi Mungu atamchagua mtu mmoja katika u…

Makundi : Mambo yaliyo bora. · Ubora wa Tauhiid. · Akida- Itikadi- · Mambo mazuri na Adabu- Heshima. · Kuamini siku ya mwisho

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله وبحمده Gloire et louange à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56