Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi hakika nim…

Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi hakika nim…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: Atakayemfanyia u…

عَنْ أَبِي هُرَيْرَة رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُول اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إنَّ اللَّهَ تَعَالَى قَالَ: مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقْد آذَنْتُهُ بِالحَرْبِ، وَمَا تَقَرَّبَ إلَيَّ عَبْدِي بِشَيْءٍ أَحَبَّ إلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُ عَلَيْهِ، وما يَزَالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إلَيَّ بِالنَّوَافِلِ حَتَّى أُحِبَّهُ، فَإِذَا أَحْبَبْتُهُ كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بِهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بِهِ، وَيَدَهُ الَّتِي يَبْطِشُ بِهَا، وَرِجْلَهُ الَّتِي يَمْشِي بِهَا، وَإِنْ سَأَلَنِي لَأُعْطِيَنَّهُ، وَلَئِنْ اسْتَعَاذَنِي لَأُعِيذَنَّهُ».

Maelezo ya hadith: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: Atakayemfanyia u…

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika hadithil-Qudsi ya kwamba Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka alisema: Atakayemuudhi kipenzi miongoni mwa vipenzi vyangu na akamkasirisha na akamchukiza basi nitakua nimemjulisha na nimemtangazia uadui. Walii (Kipenzi): Ni muumini mchamungu, na kwa kadiri itakavyokuwa imani na uchamungu kwa mja ndivyo inavyokuwa nafasi yake ya kupendwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hajawahi kujiweka karibu Muislamu kwa jambo analolipenda zaidi Mwenyezi Mungu kuliko lile alilomfaradhishia na kumuwajibishia kama kufanya ibada na kuacha maharamisho, na hatoacha Muislamu kujiweka karibu kwa Mola wake Mlezi kwa ibada za sunna pamoja na faradhi mpaka atayapata mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu akimpenda basi yeye huwa msimamizi wake katika viungo hivi vinne: Anamsimamia katika masikio yake, hayatosikia ila yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu. Na anamsimamia katika macho yake, hatotazama ila yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu kuyatazama na kuyaridhia. Na anamsimamia katika mkono wake, hatofanya kwa mkono wake ila yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu. Na atamsimamia katika mguu wake, hatokwenda ila katika yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu, na hatokwenda mbio ila katika yale yenye kheri. Na pamoja na hayo, akimuomba Mwenyezi Mungu chochote basi Mwenyezi Mungu atampa alichoomba, anakuwa ni mtu mwenye kujibiwa dua, na akitaka ulinzi kwa Mwenyezi Mungu na akaomba hifadhi kwake kwa kutaka alindwe, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamlinda na kumhami na yale anayoyaogopa.

Mafunzo: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: Atakayemfanyia u…

Makundi : Akida- Itikadi- · Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka · Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله وبحمده Gloire et louange à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56