Ewe baba yangu mdogo, sema: Laa ilaaha illa llaahu (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki…

Islam > Sw > Hadith > Quran tukufu na elimu zake > Ewe baba yangu mdogo, sema: Laa ilaaha illa llaahu (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki…

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Ewe baba yangu mdogo, sema: Laa ilaaha illa llaahu (Hap…

عن سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيَّبِ، عَنْ أَبِيهِ قَالَ: لَمَّا حَضَرَتْ أَبَا طَالِبٍ الْوَفَاةُ، جَاءَهُ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم فَوَجَدَ عِنْدَهُ أَبَا جَهْلٍ وَعَبْدَ اللهِ بْنَ أَبِي أُمَيَّةَ بْنِ الْمُغِيرَةِ، فَقَالَ: «أَيْ عَمِّ، قُلْ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، كَلِمَةً أُحَاجُّ لَكَ بِهَا عِنْدَ اللهِ»، فَقَالَ أَبُو جَهْلٍ وَعَبْدُ اللهِ بْنُ أَبِي أُمَيَّةَ: أَتَرْغَبُ عَنْ مِلَّةِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، فَلَمْ يَزَلْ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَعْرِضُهَا عَلَيْهِ، وَيُعِيدَانِهِ بِتِلْكَ الْمَقَالَةِ، حَتَّى قَالَ أَبُو طَالِبٍ آخِرَ مَا كَلَّمَهُمْ: عَلَى مِلَّةِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، وَأَبَى أَنْ يَقُولَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: «وَاللهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ مَا لَمْ أُنْهَ عَنْكَ»، فَأَنْزَلَ اللهُ: {مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَنْ يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ} [التوبة: 113]، وَأَنْزَلَ اللهُ فِي أَبِي طَالِبٍ، فَقَالَ لِرَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم: {إِنَّكَ لا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَكِنَّ اللهَ يَهْدِي مَنْ يَشَاءُ} [القصص: 56].

Maelezo ya hadith: Ewe baba yangu mdogo, sema: Laa ilaaha illa llaahu (Hap…

Aliingia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa Ami yake Abuu Twalib akiwa katika hali ya kukaribia kufa, akasema kumwambia: Ewe Ami yangu sema "Laa ilaaha illa llaah", neno ambalo nitakutolea ushahidi kwalo mbele ya Allah, Abuu Jahali na Abdallah Bin Abiiy Umaiyya wakasema: "Wewe Abuu Twalib!, unaacha mila ya baba yako Abdul Muttwalib?! ambayo ni kuabudu masanamu, wakaendelea kumwambia hivyo mpaka akasema neno lake la mwisho alilowaambia kuwa: Niko katika mila ya Abdul Muttwalib, mila ya ushirikina na kuabudu masanamu, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Nitakuombea msamaha madam sijakatazwa na Mola wangu kuhusu hilo, ikateremka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Haipasi kwa Nabii na wale walioamini kuwatakia msamaha washirikina, hata kama watakuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa Motoni" [Attauba: 113], Na ikateremka kumuhusu Abuu Twalib kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika wewe, humuongoi, unayependa aongoke. Lakini Mwenyezi Mungu, Anamuongoa Anayemtaka. Na Yeye Ndiye Anayemjua zaidi anayefaa kuongoka". Kwani hakika wewe humuongoi umpendaye kumuongoa, bali jukumu lako ni kufikisha, na Allah anamuongoa amtakaye.

Mafunzo: Ewe baba yangu mdogo, sema: Laa ilaaha illa llaahu (Hap…

Makundi : Qur'an tukufu na Elimu zake · Tafsiri ya Qur'an. · Kulingania na kuelekeza kwa Mungu. · Da'awa na (kujitolea) kuamrisha mema na kukataza mabaya

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله Gloire à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56