Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo kinga ya jambo langu

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi elimu ya dua na dhikri mbali mbali > Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo kinga ya jambo langu

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo…

Maelezo ya hadith: Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo…

Aliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa dua iliyokusanya ndani yake misingi ya tabia njema alizotumwa kuzitimiliza; nazo ni kutengenezewa dini, na dunia, na Akhera, akachota kutoka katika matamshi haya mafupi kutengemaa kwa mambo makubwa matatu, na akaanza na kutengemaa kwa dini, ambayo ndiyo sababu ya kutengemaa hali ya Dunia na Akhera, akasema:

"Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu" Kwa kuniafikisha kusimamia adabu zake kwa namna iliyokamilika na kutimia zaidi.

"Ambayo ndiyo ngome ya jambo langu" Na iwe hifadhi kwa mambo yangu yote, ikiwa dini yangu itaharibika basi yataharibika mambo yangu, na nitapata hasara na kutoka patupu, na kwakuwa hakuwezi kutimia kutengemaa kwa dini inayotakiwa isipokuwa kwa kutengemaa dunia, akasema:

"Na unitengenezee dunia yangu" Kwa kunipa afya ya mwili na amani, na riziki, na mke mwema, na kizazi kizuri na yale ninayoyahitaji, na yawe ya halali, na yanisaidie katika kukutii, kisha akataja udhuru katika kuomba kwake kutengemaa kwake; kwa kusema:

"Ambayo kuna maisha yangu" Na mahala pa kuishi kwangu na muda wa uhai wangu.

"Na unitengenezee Akhera yangu ambayo ndiyo marejeo yangu" Na kurejea kwangu ili kukutana na wewe, na hii ni kwa kutengemaa kwa matendo, na Mwenyezi Mungu kumuwezesha mja katika ibada na ikhlasi, na kuupata mwisho mwema.

Na akapangilia rehema na amani ziwe juu yake Akhera baada ya dunia; kwa sababu ya kwanza ndio sababu ya kutengemaa ya pili, atakayekuwa na msimamo katika dini yake kwa namna atakavyo Mwenyezi Mungu, basi Akhera yake itanyooka na atapata furaha ndani yake.

"Na uufanye uhai" Yaani: Na kurefushwa kwa umri "Kuwa ni ziada kwangu katika kila kheri" Ili nizidishe amali njema, "Na uyafanye mauti" na kuharakishwa kwake "Raha kwangu kutokana na kila shari" Na fitina na mitihani na majaribu kwa maasi na kughafilika, na ili iwe ni sababu ya kuepukana na matatizo ya Dunia na shida zake, na kupatikana kwa raha.

Mafunzo: Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo…

Makundi : Fiq'hi -Elimu- ya Dua na Dhikri mbali mbali. · Dua zilizopokelewa toka kwa mtume. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
الحمد لله Louange à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56