Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na ujinga wangu, na ubadhirifu wangu kati…

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi elimu ya dua na dhikri mbali mbali > Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na ujinga wangu, na ubadhirifu wangu kati…

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na uji…

Maelezo ya hadith: Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na uji…

Ilikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake zilizokusanya mambo mengi ni kauli yake:

"Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe makosa yangu" "na dhambi zangu", na yale yaliyotokea kwangu pasina kujua.

"Na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote" na uzembe wangu na kuvuka kwangu mipaka.

"Na yale uyajuayo kutoka kwangu" Uliyoyajua ewe Mwenyezi Mungu lakini mimi nimeyasahau.

"Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe makosa yangu na makusudi yangu" Na yale yaliyotokea kwa makusudi na kwa kujua kwangu kuwa ni dhambi.

"Na niliyodhamiria na yale ya mzaha" Na yale yaliyotekea kwa mzaha, na yale yaliyotokea katika hali zote mbili.

"Na hayo yote toka kwangu" Kiasi kwamba yote yaliyotajwa yamekusanya madhambi na aibu zote.

"Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe niliyoyatanguliza" Katika yale yaliyopita, "Na yale niliyoyachelewesha" Katika yale yatakayokuja.

"Na yale niliyoyafanya kwa siri" niliyoyaficha "Na niliyoyatangaza" Na kuyaonyesha wazi.

"Wewe ndiye muwahishaji na wewe ndiye mcheleweshaji" Unamtanguliza umtakaye katika viumbe wako katika rehema zako kwa kumpa taufiki katika yale unayoyaridhia, na wewe ndiye unayemchelewesha umtakaye katika hilo, kwa kumnyima uwezo, hakuna wa kuyapeleka mbele uliyoyachelewesha, na wala hakuna kuyachelewesha mambo uliyoyawahisha.

"Na wewe juu ya kila kitu ni muweza" Yaani: Unauwezo uliokamilika na maamuzi timamu, mfanyaji pasina kizuizi cha yote uyatakayo.

Mafunzo: Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na uji…

Makundi : Fiq'hi -Elimu- ya Dua na Dhikri mbali mbali. · Dua zilizopokelewa toka kwa mtume. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
لا إله إلا الله Pas de divinité sauf Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56