Hivi nisikuelezeni lililo bora kuliko daraja ya swaumu na swala na sadaka?
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu kuhusu familia > Hivi nisikuelezeni lililo bora kuliko daraja ya swaumu na swala na sadaka?
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Abu Daud na Tirmidhiy
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Hivi nisikuelezeni lililo bora kuliko daraja ya swaumu…
Maelezo ya hadith: Hivi nisikuelezeni lililo bora kuliko daraja ya swaumu…
Aliwauliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake: Je, nikuelezeni lililo bora kuliko kuzidisha ibada za sunna kama swaumu na swala na sadaka? Wakasema: Ndio. Akasema: Ni kuwapatanisha waliogombana kwani ugomvi huleta mfarakano na kujitenga na kuchukiana na kupeana migongo kati ya watu, kwani yanayoambatana na kuharibika kwa mahusiano baina ya watu miongoni mwa chuki ndio jambo ambalo katika tabia zake huangamiza na kuing'oa dini na dunia kama wembe unavyong'oa nywele.
Mafunzo: Hivi nisikuelezeni lililo bora kuliko daraja ya swaumu…
- Muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kuwauliza Maswahaba zake na kuwatia shauku ya kujua jawabu.
- Amesema Al-Twayyibi: Himizo na hamasa ya kusuluhisha baina ya watu na kujiepusha na kuwavuruga; kwa sababu kutengemaa ndio sababu ya kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu na kutofarakana baina ya Waislamu, na kuharibu mahusiano ni pengo katika dini, na atakeyejitosa kulirekebisha na kuondoa uharibifu wake atapata daraja la juu zaidi ya lile analolipata mfungaji mwenye kusimama usiku mwenye kujishughulisha na nafsi yake pekee.
Makundi :
Fiq'hi- ufahamu- kuhusu familia.
· Jamii ya Kiislamu
· Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha
· Matendo ya moyoni.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
أستغفر الله
Je demande pardon à Allah