Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akifungua swala kwa takbira (Allaahu Akbaru) n…

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akifungua swala kwa takbira (Allaahu Akbaru) n…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akifungua s…

Maelezo ya hadith: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akifungua s…

Ameeleza Mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake sehemu ya swala ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba alikuwa akifungua swala yake kwa takbira ya kufungua swala, akisema: "Allaahu Akbaru", na akifungua kisomo kwa suratul Faatiha. "Alhamdulillaah Rabbil A''alamiin..." Na alikuwa anaporukuu baada ya kisimamo, hainui kichwa chake na wala hakishushi wakati wa rukuu, bali anakifanya kilingane sawa kikiwa kimenyooka, na akinyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu ananyooka wima kabla hajasujudu, na akinyanyua kichwa chake kutoka katika sijida ya kwanza, hasujudu sijida ya pili mpaka atuliazane akiwa amekaa. Na alikuwa akikaa baada ya kila rakaa mbili kwa ajili ya tahiyatu, na anasema: "Attahiyyatu lillaahi was swalawaatu wat twayyibaatu...", na alikuwa anapokaa baina ya sijida mbili au kwa ajili ya tahiyatu analaza mguu wake wa kushoto na kuukalia, na anasimamisha mguu wake wa kulia. Na anamkataza mwenye kuswali kukaa ndani ya swala yake kama mkao wa Shetani, nao ni kulaza miguu yake yote miwili katika Ardhi, na kukaa kwa pande zake mbili za nyuma, au kuambatanisha makalio yake na Ardhi na akasimamisha miguu yake na kuweka mikono yake katika Ardhi kama anavyoitandaza mbwa, au akalaza mwenye kuswali mikono yake kwa kuinyoosha katika sijida kama anavyoilaza mnyama mkali. Na alikuwa akihitimisha swala yake kwa salamu: "Assalaam alaikum warahmatullah" upande wa kulia mara moja na mara nyingine upande wa kushoto.

Mafunzo: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akifungua s…

Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Sala. · Fiq'hi na misingi yake. · Sifa za Swala. · Makosa ya wenye kusali.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
أحدب متناقص Gibbeuse Décroissante Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
حسبنا الله ونعم الوكيل Allah nous suffit, quel excellent protecteur

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56