Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi akioshe mara saba
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi akioshe mara saba
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi ak…
Maelezo ya hadith: Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi ak…
Aliamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake chombo hicho kioshwe mara saba ikiwa mbwa ataingiza ulimi wake ndani yake, mara ya kwanza iwe kwa mchanga, ili yaje maji baada yake, hivyo usafi kamili utakuwa umepatikana kutokana na najisi yake na madhara yake.
Mafunzo: Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi ak…
- Mate ya mbwa ni najisi tena ni najisi nzito.
- Mbwa kulamba katika chombo, kunakitia najisi chombo hicho, na kunanajisisha maji yaliyoko ndani yake.
- Kusafisha kwa udongo na kurudia mara saba hii ni maalum kwa kusafisha pale atakapo lamba, lakini si katika mkojo wake na uchafu wake na vyote atakavyovichafua mbwa.
- Jinsi ya kuosha chombo kwa udongo: Ataweka maji ndani ya chombo na kuongeza udongo ndani yake, kisha atasafisha chombo kwa mchanganyiko huu.
- Maana ya dhahiri ya Hadith ni kuwa hadithi hii inajumuisha mbwa wote, hata mbwa ambao sheria imeruhusu kufugwa, kama vile kuwinda, kulinda, na mbwa wa mifugo.
- Sabuni na majani ya miti havichukui nafasi ya udongo; Kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliweka sharti la kutumia udongo.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Twahara - usafi-
· Fiq'hi na misingi yake.
· Kuondoa Najisi.
· Vyombo.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
لا حول ولا قوة إلا بالله
Pas de force ni de puissance sauf en Allah