Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Mambo ya kimaumbile ni matano: Kutairi, na kunyoa sehemu za siri, na kupunguza masharubu, …
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureAmebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mambo matano katika dini ya Uislamu na sunna ya Mitume:
La kwanza: Kutairi, nako ni kukata ngozi iliyozidi juu ya kichwa cha dhakari kwa mwanaume, na kukata kingozi katika tupu ya mwanamke juu ya malaha palipo tundu la uke.
La pili: Kunyoa sehemu za siri, nako ni kunyoa nywele za kinena zinazozunguka tupu ya mbele.
La tatu: Kupunguza masharubu, nako ni kupunguza kilichoota juu ya mdomo wa juu wa mwanaume mpaka mdomo uonekane wazi.
La nne: Kupunguza kucha.
La tano: Kunyofoa nywele za kwapa.
Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Twahara - usafi- · Fiq'hi na misingi yake. · Sunna za Kimaumbile.