Atakayeacha Ijumaa tatu kwa kuzipuuzia; Mwenyezi Mungu hupiga muhuri katika moyo wake
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Atakayeacha Ijumaa tatu kwa kuzipuuzia; Mwenyezi Mungu hupiga muhuri katika moyo wake
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na Ahmad
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Atakayeacha Ijumaa tatu kwa kuzipuuzia; Mwenyezi Mungu…
Maelezo ya hadith: Atakayeacha Ijumaa tatu kwa kuzipuuzia; Mwenyezi Mungu…
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoacha swala ya Ijumaa, na kwamba mwenye kuacha swala ya Ijumaa mara tatu kwa kupuuza na uzembe pasina udhuru basi Mwenyezi Mungu atapiga na kufunika juu ya moyo wake na kizibo kinachozuia kuingia kheri yoyote ndani ya nafsi yake.
Mafunzo: Atakayeacha Ijumaa tatu kwa kuzipuuzia; Mwenyezi Mungu…
- Ameeleza bin Mundhiri kuwa kuna makubaliano ya wanachuoni wote kuwa swala ya Ijumaa ni faradhi ya lazima kwa kila mtu.
- Ahadi mbaya kwa atakayeacha swala ya Ijumaa kwa kupuuza, kwamba Mwenyezi Mungu atapiga muhuri juu ya moyo wake.
- Atakayeacha swala ya Ijumaa kwa dharura huyu haingii katika ahadi hii mbaya.
- Amesema Shaukani: Kauli yake: (Ijumaa tatu), inategemea maana mbili, kuacha kwa ujumla sawa sawa zimefuatana Ijumaa hizo au zimetofautiana, hata akiacha katika kila mwaka Ijumaa moja basi Mwenyezi Mungu angepiga muhuri juu ya moyo wake baada ya Ijumaa ya tatu, na ndivyo hadithi inavyoonyesha, na maana ya pili nikuwa inakusudiwa Ijumaa tatu mfululizo.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Sala.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Swala ya Ijumaa
· Virtue of Friday
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
سبحان الله وبحمده
Gloire et louange à Allah