Ewe Bilali, hebu nihadithie kuhusu amali yenye matarajio makubwa zaidi uliyowahi kuifanya …
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Ewe Bilali, hebu nihadithie kuhusu amali yenye matarajio makubwa zaidi uliyowahi kuifanya …
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Ewe Bilali, hebu nihadithie kuhusu amali yenye mataraji…
Maelezo ya hadith: Ewe Bilali, hebu nihadithie kuhusu amali yenye mataraji…
Aliona Mtume rehema na amani ziwe juu yake usingizini kuwa yuko Peponi, akasema kumwambia Bilal bin Rabaha: Nieleze kuhusu amali yoyote ya sunna yenye matarajio makubwa uliowahi kuifanya ndani ya Uislamu? kwani mimi nilisikia sauti ya chini ya viatu vyako wakati wa kuvitikisa kwa kutembea mbele yangu Peponi. Bilal akasema: Sikuwahi kufanya amali yoyote yenye matarajio makubwa yoyote kwangu zaidi yakuwa sijawahi kutengukwa udhu wakati wowote iwe usiku au mchana isipokuwa ninatawadha, kisha ninaswali kwa ajili ya Mola wangu kwa udhu huo swala za sunna zisizo na mpaka kiasi nilichoandikiwa kuswali.
Mafunzo: Ewe Bilali, hebu nihadithie kuhusu amali yenye mataraji…
- Ubora wa amali aliyoisema Bilal radhi za Allah ziwe juu yake, nayo ni swala kila anapopata twahara na akatia udhu, na kwamba hiyo ni miongoni mwa amali inayotarajiwa zaidi, na ni sababu ya kuingia Peponi.
- Sunna ya kuswali baada ya kila udhu.
- Kiigizo na mlezi kuuliza matendo ya mwanafunzi wake; ili amhimize kudumu nayo kama ni matendo mazuri, na kama si hivyo basi amkataze.
- Ushahidi kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Bilal radhi za Allah ziwe juu yake kuwa yeye ni katika watu wa peponi.
- Swali hili lilikuwa wakati wa swala ya Alfajiri, na kwa hili ni ishara kuwa tukio hili lilitokea katika ndoto yake rehema na amani ziwe juu yake, na ndoto za Manabii ni kweli.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Sala.
· Akida- Itikadi-
· Fiq'hi na misingi yake.
· Swala ya Kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.
· Kuamini siku ya mwisho
· Maisha ya Akhera.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
سبحان الله وبحمده
Gloire et louange à Allah