Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo yatakayowaingiza watu peponi …

Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo yatakayowaingiza watu peponi …

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad

Ni nzuri (Hasan) na ni sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu…

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: سُئِلَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ أَكْثَرِ مَا يُدْخِلُ النَّاسَ الْجَنَّةَ، فَقَالَ: «تَقْوَى اللهِ وَحُسْنُ الْخُلُقِ»، وَسُئِلَ عَنْ أَكْثَرِ مَا يُدْخِلُ النَّاسَ النَّارَ فَقَالَ: «الْفَمُ وَالْفَرْجُ».

Maelezo ya hadith: Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu…

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa sababu kubwa zinazowapeleka watu peponi ni mbili:

Uchamungu na tabia njema.

Uchamungu: Ni mtu kuweka kinga kati yako na adhabu ya Mwenyezi Mungu, nako ni kwa kufanya maamrisho yake na kuyaepuka makatazo yake.

Na tabia njema: Inakuwa kwa kukunjua uso na kutenda wema na nakujizuia na kero.

Na sababu kubwa zinazowaingiza watu motoni ni mbili nazo ni:

Ni ulimi na utupu.

ulimi miongoni mwa maasi yake: Ni uongo, kusengenya, kuchonganisha, na mengineyo.

Na utupu katika maasi yake: Ni zinaa na kulawiti na mengineyo.

Mafunzo: Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu…

Makundi : Fiq'hi ya Tabia. · Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Tabia njema. · Sifa za pepo na moto. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
أستغفر الله Je demande pardon à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56